Parvovirus Infection/Parvo (new)

Ufahamu Ugonjwa wa Canine Parvovirus

Unaoweza kupoteza maisha ya Mbwa wako ndani ya muda mfupi
Mbwa ni mnyama kama wanyama wengine ambao huweza kupata magonjwa mbalimbali ambayo hupelekea kufa au kuwapa vilema vya maisha.
Mbwa ni kama binadamu yoyote tu ambaye akishambuliwa na magonjwa basi anaweza kuwa dhaifu na kupelekea kupoteza maisha au kupona lakini pia ni wanyama kama binadamu tu wengine ambao hata wakipatwa na baadhi ya magonjwa basi wanaweza kustahimili na kupona kabisa.
Basi leo tutaangalia baadhi ya magonjwa yanayowapata viumbe hivi vinavyopendwa sana na rafiki mkubwa wa binadamu.
Kama ilivyo kwa wanyama wengine na binadamu ugonjwa uanza kuonekana kutokana na dalili flani ambapo ndio zinakupa taarifa za kuhisi kuwa mnyama huyu ni mgonjwa.
Lakini kuna baadhi ya magonjwa ukiona dalili zake basi unajua kabisa kuwa ishatafuna sehemu kubwa na kupona ni majaaliwa na hali ipo hivyo hivyo kwa wanyama kama Mbwa.
Tuanze na Huu leo


1:Parvovirus Infection (Kwa kifupi uitwa Parvo)

Ugonjwa huu ni ugonjwa unaosababishwa na Virusi ambapo mara nyingi hushambulia mbwa wadogo wenye umri wa kuanzia wiki sita mpaka miezi sita. Ugonjwa huu ni moja ya ugonjwa mbaya sana kwa mbwa kwasababu unapomuingia tu basi matumaini ya kupona kwa mbwa huyo ni madogo sana kwasababu ni ugonjwa ambao ukimpata mbwa ndani ya masaa 24 unaweza kupelekea kifo kwa mbwa huyo. Ugonjwa huu husambulia sana mapigo ya moyo na kupelekea mapigo ya moyo ya mbwa huyo kwenda mbio sana, na kumfanya hapoteze hamu ya kula, joto kushuka sana.

…………………………………………………………………………………………………………………

Share Now

Related posts