MAGONJWA YA NGURUWE CHANJO,KINGA NA TIBA (new) I Mshindo Media

MAGONJWA HATARI KWA NGURUWE. Leo tutaangazia magonjwa mawili ya nguruwe ambayo ni. 1. Kimeta ( Anthrax) 2. Ugonjwa wa ngozi. 1. Kimeta ( Anthrax) Ugonjwa huu husababishwa na bacteria wajulikanao kama Bacillus anthracis, wadudu hawa wanabaki kuwa hai kwa muda mrefu na wanaweza kuwa kwenye udongo wakiwa hai kwa kipindi cha miaka mingi Dalili za ugonjwa. -uvimbe kwenye shingo/mgongo. -Homa -Kutoa kinyesi chenye damu. -Kupumua kwa tabu -Kifo cha ghafla -Mnyama aliyekufa kwa kimeta damu haigandi ( Huendelea kutoka) katika maeneo ya wazi kama puani, mdomoni na masikioni na hata…