MAGONJWA YA NGURUWE CHANJO,KINGA NA TIBA (new) I Mshindo Media

MAGONJWA HATARI KWA NGURUWE.

Leo tutaangazia magonjwa mawili ya nguruwe ambayo ni.

1. Kimeta ( Anthrax)

2. Ugonjwa wa ngozi.

1. Kimeta ( Anthrax)

Ugonjwa huu husababishwa na bacteria wajulikanao kama Bacillus anthracis, wadudu hawa wanabaki kuwa hai kwa muda mrefu na wanaweza kuwa kwenye udongo wakiwa hai kwa kipindi cha miaka mingi

Dalili za ugonjwa.

-uvimbe kwenye shingo/mgongo.

-Homa

-Kutoa kinyesi chenye damu.

-Kupumua kwa tabu

-Kifo cha ghafla

-Mnyama aliyekufa kwa kimeta damu haigandi ( Huendelea kutoka) katika maeneo ya wazi kama puani, mdomoni na masikioni na hata nzi hawasogelei mzoga wake

Kinga na tiba.

-Nguruwe wapatiwe chanjo ya ugonjwa huu.

-ugonjwa huu unaweza kutibiwa kwa madawa ya antibiotics, unaweza ukatumia dawa aina ya Penisilin au Oxytetracycline.

-Nguruwe mgonjwa asichinjwe na aliyekufa asipasuliwe.

-Toa taarifa kwa mtaalamu wa mifugo haraka.

Zingatia: Nguruwe alie kufa kwa kimeta usimshke kabisa kwa sababu hata binadamu anaweza kuambukizwa ugonjwa huu, chimba shimo mbali na watu mwagia mafuta ya taa ndani ya hilo shimo kisha fukia mzoga.

2. Ugonjwa wa ngozi.

Ugonjwa huu hutokana na ukosefu wa vitamini. Pia unaweza kuenezwa na chawa, viroboto, nzi na utitiri

Dalili za ugonjwa.

-Kujikuna mara kwa mara.

-Uvimbe kwenye ngozi.

-Hushindwa kula vizuri.

-Kupungua uzito.

Tiba na kinga

-Lisha nguruwe chakula chenye vitamini na madini ya kutosha.

-Ogesha nguruwe vizuri.

-Tumia dawa ya kuua wadudu kama viroboto, utitiri, chawa na nzi.

-Zingatia usafi wa banda

Zifuatazo ni dalili za nguruwe mgonjwa;-

·         haonyeshi dalili za kupenda chakula

·         anaweza kuhema kwa kasi dalili ya homa

·         macho makavu

·         ngozi kavu

·         anakua anajitenga

·         masikio kulala

·         kwenye ngozi nyeupe ngozi inaweza kua nyekundu

·         mkia kua mwembamba

·         kuhalisha mda mwingine kuhalisha damu

MAGONJWA YANAYO SABABISHWA NA WADUDU

Wadudu wa ndani

Minyoo ndo wadudud wakuu wanaathiri tumoni kwa nguruwe, kuna minyoo zaidi ya 30,ila minyoo ambao wanaathiri kwa wakati mwingi ni minyoo duara(round worm) na minyoo tape(tape worm).

Round worm

Hii ukaa kwenye utumbo mpana wa nguruwe na uchukua chakula kutoka kwa nguruwe hivo nguruwe anaweza kukonda.minyooo mikubwa(Ascaris lumbricoides) hii ndo inapatikana sana.minyoo  hii nimikubwa urefu wa penseli.maambukizi yanaanza pale myama anapo kula chakula chenye mayai ya monyoo hao.

DALILI

·         Kunyonyoka manyoya(anorexia).

·         Upungufu wa damu(anaemia).

·         Baadae uzito upungua.

·         Minyoo wakitibiwa wakati washakua wengi wanaweza kukata utumbo na kusababisha kifo.

KUKINGA/PREVENTION

·         Kuzuia kwa kuweka dawa kwenye chakula na kutumia vyombo visafi

·         Kuchunga kwa kutumia njia ya mzunguko na kutibu nyasi

·         Kuwatenga watoto na wakubwa

·         Kuwapatia dawa ya minyoo mara kwa mara

·         Muoshe jike kabla ya kuzaa

·         Unaweza kutumia miti shamba aina ya moringa

Tape worm

Hawa wanakua frat kama rebon na wanapatikana mahali tofauti tofauti dunian.hawana utumbo hivyo wanakula kupitia ngozi yao na wanachukua virutubisho.hua wanachukua folic acid na vitamin B-12 mwilini,wanaweza kusababisha sumu kwakua baada ya kula wanaacha uchafu na unakua kama mpira ambao unakaa karibu na ini.

DALILI

·         Kudumaa

·         Upungufu wa damu

·         Ngozi kubadilika nakua mbaya

KINGA/PREVENTION

·         Kuwapa dawa ya minyoo

·         Hakikisha wanao hudumia nguruwe wawe wanatumia choo na kusafisha

WADUDU WA NJE

Wadudu wa nje inahusisha mange.lies na myiasis

Mange

Husababishwa na wadudu wanao itwa mites wanaishi kwenye ngozi ya nguruwe maeneo ya machoni, masikioni,miguuni  na shingoni

DALILI

·         Nguruwe anakua anjikuna kuna kwenye ukuta kwenye miguu,masikio,macho na masikio

·         Ngozi inakua na mabaka kama vibarango na mistali mistali mwenkundu kama vidonda

·         Manyoya hua yamevurugika

·         Ngome anakua hatulii

·         Vifo

·         Na kupungukiwa damu kwa watoto

KINGA/PREVENTION

·         Osha nguruwe mara mbili kwa wiki

·         Madume wanatakiwa kuoshwa pia

·         Wape dawa kila nguruwe anapoingia shambani kwako

·         Usafi wa banda

TIBA/TREATMENT

·         Unaweza kuwaosha  pia kwa maji safi na sabuni

·         Unaweza kuwaosha kwa  organophosphate

·         Unaweza kuwachoma Ivermectin kwakua inasaidia sana

CHAWA

Hawa wanakua wananyonya damu na dalili zake ni upungufu wa damu na pia mnyama anakua na madoa mekundu mwilini. Na pia unaweza kutibu Kwa kutumia viuadudu (insecticide) benzene hexachloride ndo hua inatumika kuua chawa.

MYIASIS

Huu ni ugonjwa unaosababishwa na nzi wanao taga mayai kwenye vidonda,mayai hayo hukua hadi kufikia hatua ya kua nzi mkubwa na husababisha kidonda kua kikubwa zaidi.

Kidonda hua kichafu na kua kama na ukungu mweusi ambayo hayo ni mayai ya nzi,hivyo kuzuia hii unatakiwa kusafisha banda na kupunguza idadi ya  nguruwe katika banda wasisongamane

KUWAPA DAWA ZA MINYOO(DEWORMING)

Dawa za minyoo ambazo zimehakikishwa nan i salama pale zinapo pewa kutokana na maelekezo sahihi ni kama

vermectin (Ivomec®), fenbendazole (Safe-Guard®), levamisole (Tramisol®, Levasole®), pyrantel (Banminth®), dichlorvos (Atgard®) na piperazine.

Unaweza kupanga ratiba ya kuwapa dawa zaminyoo na ukapanga na mtalaamu ili kua anawapa chanjo ifikapo siku sahihi

·         Dume/Boars – kila miezi 6 months

·         Jike/Sows – wiki 2 kabla ya kuzaa na baada ya kuwatenga watoto

·         Watoto/Piglets – wiki 1 baada ya kuwatenga

·         Wanao nenepeshwa/Fatteners – wiki moja baada ya kuwatenga na miezi mitatu badae

·          Gilts – wiki 1 aada ya kuwatenga na unaweza kurudia miezi mitatu badae

DAWA ZA WADUDU WANAO JITOKEZA MARA KWA MARA

MINYOO NA HATUADAWA
Ascarids(adult)Zote
Ascarids(hatua ya larva wanao hama)Fenibendazole
Ascarids(hatua ya larva waalibifu)Fenibendazole.pyrantel
whipwormsFeniendazole, , dichlorvos
Noduluar wormZote
Minyoo ya figo(wakubwa)Fenbendazole, ivermectin, levamisole
Minyoo wa figo(larva katika ini)Fenbendazole, levamisole
strongloydesFenbendazole
Levamisole, ivermectin
Share Now

Related posts