Contagious ecthyma (new) I Mshindo Media

Ugonjwa huu una majina mengi ya kitaalamu: contagious pustular dermatitis, contagious ecthyma, infectious labial dermatitis, ecthyma contagiosum, thistle disease and scabby mouth.

–huu ugonjwa unaowapata mbuzi na kondoo, husababishwa na virusi vinavyoitwa parapox virus.

Virusi hivi huishi kwenye mazingira kama kuta za banda, vyombo vya chakula, kwenye malisho n.k na huweza kukaa mwezi, mwaka na zaidi.

 Uenezwaji

Virusi hawa humpata mnyama kupitia sehemu zilizo wazi kwa kuumia kama kidonda na mara nyingi huwapata mbuzi sababu wanapenda kula miba inayo pelekea kupata majeraha sehemu za mdomo.

-pia watoto wa mbuzi wanao nyonya kama ni wagonjwa huweza kuambukiza mama zao.

-kugusana na mnyama anae umwa.

Dalili

Dalili kuu ni vidonda mdomoni

-pia huweza kuwa na vidonda kwenye matiti na maskioni.

Kinga na tiba

Chanjo dhidi ya ugonjwa huu ipo na ni muhimu kwasababu haipo tiba maalumu dhidi ya ugonjwa huu, hivyo pale unapo tokea antibiotics hutumika na njia zingine asilia.

–Pia wanyama wagonjwa watengwe(quarantine) mbali na wanyama wengne ili kuepusha maambukizi.

NB:

Ugonjwa huu huweza kuambukizwa kutoka kwa mnyama kwenda kwa binadamu hivyo unapaswa kujikinga unapo hudumia wanyama wagonjwa.

Share Now

Related posts