Ufugaji bora wa mbuzi (new) I Mshindo Media

UFUGAJI BORA WA MBUZI

Mbuzi ni wanyama ambao wanaweza kufugwa kwa gharama nafuu pia ni wavumilivu wa ukame na maradhi tofauti na ngo’mbe kwa kua wana umbile dogo wanaweza kufugwa katika eneo dogo na nguvu kazi ndogo na hata kwa wenye kipato kidogo.Mbuzi  wanaweza kufugwa kwa ajili ya nyama/maziwa/ngozi/sufi na mazaomengine kama mbolea kwa matumizi ya familia na kuongeza kipato.

NAMNA BORA YA UFUGAJI:-
Wafugwe kwenye banda bora
Chagua kulingana na sifa zao na lengo la ufugaji(uzalishaji)nyama/maziwa/sufi.
Walishwe chakula sahihi kulingana na umri
Kuzingtia ushauri wa mtaalamu wa mifugo hasahasa namna ya udhibiti wa magonjwa.
Kuweka kumbukumbu za uzalishaji.
Kuzalisha nyama/maziwa/sufi bora unaokidhi mahitaji ya soko.

ZIZI/BANDA LA  MBUZI

1.Banda bora linatakiwa liwe ni lenye kuweza kuwakinga mbuzi au kondoo na mashambulizi ya wanyama wakali(hatari) na wezi.

2.Liwepo sehemu ambayo maji hayawezi kutuama.

3.Mabanda yatenganishwe kulingana na umri.

4.Liwe na ukubwa ambao linaweza kufanyiwa usafi.

UFUGAJI WA NDANI ZINGATIA HAYA 

Banda imara lenye uwezo wa kuwahifadhi kiafya,upepo/mvua n.k Lenye hewa ya kutosha Liwe na sakafu ya kichanja na sehemu ya kuwekea chakula na maji.  Liwe na vyumba tofauti kwa kuweka vijitoto/wanao ugua/wanao kua.

UJENZI WA BANDA LA MBUZI
Banda lijengwe kwa kutumia vifaa vilivyopo eneo husika na kwa kuzingatia uwezo wa mfugaji.
Kuta ziwe imara na zinazo ruhusu mwanga na hewa ya kutosha.
Mlango uwe na ukubwa wa 60X150 sentimeta.
Sakafu iwe ya udongo/zege ya kichanja unaweza kutumia mabanzi/mianzi na iruhusu kinyesi na mikojo kudondoka chini
Chumba cha majike na vitoto kiwe na sentimeta 1.25 kati ya fito na fito au papi na papi,chumba cha mbuzi/kondoo wakubwa kiwe na sentimeta 1.9kati ya mbao na mbao.

UCHAGUZI WA MBUZI WA KUFUGA:-
Lengo ni kuboresha uzalishaji na kupata kizazi bora kuna aina nyingi za mbuzi wa kufugwa kulingana na mazingira na mahitaji ya mfugaji.Uchaguzi unaweza kufanyika kuangalia umbile,uzalishaji na kumbukumbu za wazazi kama vile umbo kubwa,ukuaji wa haraka uwezo wa kutunza vitoto na kutoa maziwa mengi

SIFA ZA ZIADA:-
Miguu ya nyuma iliyo nyooka na yenye nafasi kwa ajili ya kiwele,kiwele kiwe kikubwa na chuchu ndefu zilizo kaa vizuri.

SIFA ZA DUME:-

  • Miguu iliyo nyooka na yenye nguvu
  • Mwenye kokwa mbili zilizo kaa vizuri a kunyooka
  • Mwenye uwezo na nguvu za kupanda
  • Asiwe na ulemavu

UTUNZAJI WA VITOTO:-
Hakikisha kitoto kinapata maziwa ya mwanzo(dang’a)siku za kwanza-3.
Kama kinanyweshwa kipewe lita 0.7-0.9 kwa siku maziwa haya ni bora kwa kuwa yana viinilishe na kinga dhidi ya magonjwa
Kama mama hatoi maziwa au amekufa mbuzi mwingine anae nyonyesha anaweza kusaidia kukinyonyesha.
Kitoto kinyonye kwa wiki12-16 baada ya wiki2 kuzaliwa pamoja na maziwa apewe chakula kingine kama nyasi ili akuze
tumbo lake pia apewe maji ya kutosha.
Aachishwe kunyonya akifikisha miezi 3
Vipewe chanjo ya magonjwa kulingana na ushauri wa mtaalam

MATUNZO MENGINE:-
Mbuzi  awekewe alama ili iwe rahisi kwa mfugaji kutunza kumbukumbu.


KUONDOA VISHINA VYA PEMBE:

-Aondolewe vishina kati ya siku 3-14 na mtaalam wa mifugo


KUHASI:

-Vitoto ambavyo havitatumika kuendeleza kizazi vihasiwe na mtaalam wa mifugo

UTUNZAJI WA MBUZI WA MIEZI4-8

Ili mbuzi aweze kukua na kupevuka mapema zingatia yafuatayo:-
Kumpatia chakula cha ziada kwa miezi 2 mfululizo kiasi cha kilo 0.2-0.7 kwa siku kuanzia anapo achishwa kunyonyesha.
Kumpatia dawa za kuzuia minyoo kama utakavyoshauriwa na mtaalam wa mifugo na aogeshwe mara kwa mara ili kuzuia magonjwa.
Kukata kwato zikikomaa.


UMRI WA KUPANDISHA:-

Wakitunzwa vizuri wanaweza kupandishwaKisasa umri wa miezi 8-12

Wa asili miezi18-24 kuzingatia afya yake na uzito wastani kilo 12.

DALILI ZA JOTO:-

  • Hutingisha mkia  
  • Hutoa ute mweupe ukeni  
  • Hufuata dume  
  • Hamu ya kula hupungua   
  • Hukojoa mara kwa marav  
  • Uke huvimba na huwa mwekundu kuliko kawaida  
  • Huangaika mara kwa mara na kupiga kelele  
  • Kwa mbuzi anayekamuliwa hupunguza kiwango cha maziwa.  
  • Mbuzi mwenye dalili hizi apelekwe kwa dume na uchunguze  tena dalili za joto baada ya siku 19-21  
  • Msimu mzuri wa kuzaa ni baada ya mvua.

UTUNZAJI WA MBUZI/KONDOO MWENYE MIMBA:-

1.     Mbuzi hubeba mimba kwa muda wa miezi 5

2.     Apewe chakula cha ziada 0.2-0.7.

3.     Apewe nyasi,miti malishi na mikunde mchanganyiko kilo 1.8-2.5 kwa siku


DALILI ZA KUKARIBIA KUZAA:-

*       Huangaika kwa kulala na kuamka mara kwa mara

*       Hujitenga na kundi na hufuata sehemu kavu na yenye kivuli

*       Hutokwa na ute mzito ukeni

*       Hupiga kelel

*       Pindi ukiona dalili hizi muandalie sehemu maalum ya kuzalia na muwekee maji ya kutosha.

UTUNZAJI WA MBUZI ANAYE NYONYESHA:-
Huhitaji chakula zaidi kwa kuzalisha maziwa  kama vile nyasi jamii ya mikunde na majani ya miti malisho kg 1.8-2.5 kwa siku ni muhimu apewe nyongeza ya 0.3-0.8 kwa kila lita inayoongezeka na maji safi na salama wakati wote


UKAMUAJI WA MAZIWA ZINGATIA HAYA:

-Sehemu ya kukamulia iwe safi na tulivu.
-Awe na afya nzuri kiwele kioshwe na maji safi ya uvuguvugu.
-Mkamuaji asibadilishwe badilishwe,awe msafi mwenye kucha fupi na asiwe na magonjwa ya kuambukiza.
-Vyombo vya kukamulia viwe safi.
Maziwa ya mwanzo yakamuliwe kuchunguza kwenye chombo maalum(strip cup) kama yana ugonjwa wa kiwele.

UTUNZAJI WA DUME BORA LA MBEGU:-
Dume la mbegu linahitaji matunzo mazuri ili liweze  kuzalisha.
Dume bora huanza kupanda likiwa umri miezi 8-10 uwiano wa dume na jike ni dume moja kwa jike 40-50.
Malisho ya kutosha na chakula cha ziada kisipungue kilo 0.2-0.7 kila siku na maji ya kutosha.
Malisho ya miti yenye lishe,jamii ya mikunde na nyasi na mabaki ya mazao pia kilo 0.45-0.9 za chakula cha ziada kulingana na uzito wake na wingi wa majike anayopanda wiki 2 kabla

Mfugo unapoonyesha dalili hizi na nyingine zisizo za kawaida muone Afisa mifugo aliyopo jirani akusaidie;·         

  • Kupumua kwa shida·         
  • Homa kali,·         
  • Kukohoa·         
  • Kutiririsha mafua·         
  • Usambaaji wa haraka na vifo vingi kwa mbuzi wa umri wowote na jinsia zote pamoja·         
  • Kutupa mimba kwa mbuzi wenye mimba·         
  • Kula kwa shida·         
  • Manyoya kunyonyoka
Share Now

Related posts