Magonjwa yanayo tibika kwa chanjo/Viral Infections (new)

Tujifunze Ugonjwa Wa Kuku Unaosababishwa Na VirusiGumboro (Ugonjwa wa Kuambukiza wa Bursar)* Ni ugonjwa unaosababishwa na virusi ambao hushambulia zaidi kuku, bata maji na bata mzinga. Kuku na bata  wadogo hadi wiki 12 ndio wanaoathirika zaidi. Jinsi Ugonjwa Unavyoenea •Chanzo cha maambukizi ni maji, chakula na vifaa/vyombo vya shambani vilivyochafuliwa na kinyesi cha kuku wagonjwa na wenye vimelea.  •Maambukizi pia huenea kupitia mfumo wa hewa, kwa vumbi lenye vimelea katika mabanda. Chukua Tahadhari Wageni, wafanyakazi na magari yanaweza kusambaza ugonjwa kutoka shamba hadi shamba au banda hadi banda.  Hii ni…

NG’OMBE WAZURI WA MAZIWA NA KUZALISHA (new) I Mshindo media

Fahamu ni aina gani ya ng’ombe wa maziwa ni bora zaidi kufuga kwa lengo la kuzalisha  Uzalishaji wa maziwa ni biashara nzuri sana na ya kuvutia ambayo huwa na faida nyingi na humfanya mfugaji kuridhika hasa kwa yule anayependa kazi hii. Hata hivyo, ni lazima kuanza kwa kuweka msingi imara hata kabla ya kufikiria ni aina gani ya mbegu utaichukua kwa ajili ya kufuga. Ni vizuri kufahamu kuwa, usimamizi ni moja ya jambo muhimu sana ambalo likifanyiwa uzembe linaweza hata kumbadilisha ng’ombe wa maziwa kuwa na uzalishaji duni kama ngo’mbe…

DAWA ZA ASILI ZA KUTIBU MAGONJWA TOFAUTI YA KUKU (new) I Mshindo Media

DAWA ZA ASILI ZA KUTIBU MAGONJWA TOFAUTI YA KUKUZipo dawa tofauti za asili zinazopatikana kirahisi kwenye mazingira ya vijijini ambazo zina uwezo wa kutibu magonjwa ya kuku. Katika mada hii taelezea baadhi ya dawa hizo. Dawa ya kutibu Homa ya Matumbo “Fowl Typhoid” ni Kitunguu swaumu Kuandaa•Chukua robo kilo ya vitunguu swaumu•toa maganda.•Kisha twanga•changanya na maji kiasi cha lita moja•chuja na kuwapa maji yake kwa muda wa juma moja.……………………………………………………………………………………………………………………………………….

Jinsi shubiri mwitu (Aloe Vera) inavyotibu magonjwa ya kuku (new) I Mshindo media

Shubiri mwitu (Aloe VERA) ni mmea ambao umekuwa ukitumika kwa kutibu magonjwa mbalimbali ya binadamu na mifugo. Mmea huu unatumika sasa kutengeneza sabuni, dawa za binadamu na wanyama na mambo mengine mengi. Na kwa sababu ya madawa mengi ya kiwandani kushindwa kutibu baadhi ya magonjwa kwa sababu wadudu wametengeza ukinzani, ipo haja kubwa ya kuweka umuhimu kwenye madawa ya asili yatokanayo na mimea. Mmea wa aloe vera unauwezo wa kutibu magonjwa ya kuku hasa coccidiosis na kwa kiasi fulani Newcastle disease. Tafiti zilifanyika kwa kutumia mti huu kutibu ugonjwa coccidiosis…

Mwongozo Wa Ufugaji Bora wa Samaki Kwenye Bwawa (new)

URUTUBISHAJI WA BWAWA LA SAMAKI KWA MBOLEA NA (MAJIVU) PAMOJA NA USAFIRISHAJI WA VIFARANGA WA SAMAKI. Kutegemea aina ya udongo, majivu ya moto huweza kutawanywa bwawani kabla ya kuingiza maji ili kupunguza Tindikali ya udongo na kuua baadhi ya wadudu walio maadui wa samaki waliopo katika eneo la bwawa.Mbolea huweza kutawanywa bwawani kabla ya kuweka maji ili kusaidia kujenga mazingira ya maji kutuama (yaani Kushikamanisha udongo).Vinginevyo, mbolea huwekwa eneo maalum (Uzio) mara baada ya maji kuingizwa bwawani ili kulirutubisha na Kuliwezesha liwe na vijimea na vijidudu vidogo vidogo vitakavyokuwa chakula…