JIFUNZE UGONJWA WA NDUI YA KUKU NA TIBA YAKE (new) I Mshindo Media

NAMNA YA KUTIBU UGONJWA WA NDUI YA KUKU KWA KUTUMIA DAWA ZA ASILI.

DALILI ZA UGONJWA WA NDUI.
· Ugonjwa wa ndui utaona kuku wako wamepata mapele kwenye kichwa yenye rangi ya kahawia, mapele hayo yanaweza kuziba mpaka macho kufanya kuku wako wasione kabisa na kusababisha kuku wako wakashindwa kula hivyo wakadhoofika kabisa na hatimaye kufa. Ugonjwa huu huwapata kuku wa rika zote lakini huathiri sana vifaranga.

Mara nyingi magonjwa ya virusi ni magonjwa ambayo hayana tiba lakini yana kinga. Wape chanjo kuku wako hasa vifaranga wanapokua wamefikia umri wa siku 56 yani wiki nane (8), na kama usipo wachanja kuku wako na kwa bahati mbaya ugonjwa huu ukaingia bandani kwako basi la kufanya ni hili hapa..
NAMNA YA KUTIBU UGONJWA WA NDUI.
Njia hii nimeshaitumia mara kadhaa pale ugonjwa ulipowapata kuku wangu na ikanipa matokeo chanya kwa asilimia 95%.
Kwanza kabisa nunua OTC 20% pamoja na vitamin, wachanganyie kuku wako kwenye maji ili kuwaepusha na magonjwa nyemelezi kwa sababu wanapokua wanashambuliwa na ugonjwa wa ndui ugonjwa wa ndui una sifa ya kupunguza sana kinga ya mwili, kinga ya mwili kwa kuku wako inashuka sana hivyo inakua rahihisi kwa kuku wako kuambukizwa magonjwa mengine, kwa hiyo unapokua unawapatia OTC 20% pamoja na VITAMIN inawasaidia kuboost kinga ya mwili..
Sasa uatafanyaje ili kutibu ugonjwa wa ndui? Kwanza kabisa tafuta mafuta ya ng’ombe yanapatikana masokoni hasa masoko makubwa makubwa unaweza ukanunua maziwa freshi ambayo hayajawekewa maji ukayagandisha alafu ile samli ya juu ukaichukua kama mafuta ya ng’ombe.

Unayafanyaje sasa hayo mafuta ya ngo’mbe, Mafuta hayo unawapakaa kuku wako maeneo ambayo yana hayo madonda. Unapaka mara mbili kwa siku asubuhi na jioni ndani ya siku mbili. Baadae yale madonda yanakua yamelainila na unaweza kuyabandua bila shida yoyota na kuku wako wanakua vizuri na wanakua wamepona.
kama kuna njia nyingine unayoitumia kutibu ugonjwa huu basi usisite kushare na wengine . Ahsante, kwa pamoja tunajenga uchumi.

……………………………………………………………………………

Share Now

Related posts