CHANJO YA NDUI (FOWL POX) new I Mshindo media

MSHINDO MEDIA Wanakupatia huduma ya kuchanja kuku wako chanjo ya NDUI (Fowl Pox)  bule kupitia website yetu hapa .
Usisubiri kuku wako waugue ndiyo uwachanje Chanjo ya Ndui.
Tuwahi mapema kuwachanja kuku wetu NDUI ili wawe na afya nzuri na tupate manufaa ya kufuga kuku.
Huduma zetu ni za uhakika na popote tutakufikia.

FAHAMU MAANA YA NDUI YA KUKU……..

Ndui ni ugonjwa unaosababishwa na virus aina ya Avipox
Virus ambao hushambulia zaidi kuku na jamii yote ya ndege, katika umri wowote wa kuku ndui inaweza ikampata kuku.

Virusi hivi vya Ndui husambaa kwa njia nyingi ikiwemo…

– Kwa njia ya kuku kudonoana.
– Kupitia ndege wa porini kwa kuingiliana vyombo vya maji na chakula.
– Pia vyombo vya maji na chakula vinavyo chafuliwa na kuku mwenye vimelea vya ugonjwa wa ndui.
– Pia maabukizi ya virus vya ugonjwa wa ndui kwa kuku husababisha kuku kudumaa na kua na ukuaji usio mzuri,kuku hupunguza kiwango cha utagaji.
– Pia virus avipoxvirus vinaweza kuishi katika mazingira kwa mda mrefu.

DALILI ZA UGONJWA WA NDUI

1. Hushambulia zaidi sehemu zilizo wazi zisizo na manyonya kwa uwepo wa vinundu(viuvimbe)vya rangi ya kahawia.
2.Kupumua kwa shida,macho ya kuku kuonekana kusinzia na kuwa na mfano wa kitu cheupe kwenye jicho,
3.Utando mweupe mdomoni, vifo vinaweza kufikia hadi 50% na zaidi.

KINGA NA TIBA

Ugonjwa wa ndui hauna tiba unashauriwa kuchanja kuku wako mapema hasa kipindi cha miezi ya joto wachanje wakiwa na umri wa wiki 6 hadi wiki 8 , tenga kuku wanao umwa ili kuzuia maambukizi kuenea.

Fukia au choma mizoga yote iliyo kufa kwa ugonjwa.

Kuku anae umwa mpatie vitamini pamoja na glucose ili kupunguza makali ya ugonjwa,pia tumia antibiotic ili kuzuia maambukizi mapya yanayo weza kujitokea.
Pia utapata ushauri wa ufugaji bora na wa Kisasa kwa kuku wako.

TUTOKOMEZE NDUI ILI KUBORESHA AFYA ZA KUKU WETU
…………………………………………………………………………………………

Share Now

Related posts