Chakula na Malisho Bora kwa Ng’ombe wa Maziwa I Mshindo media

Kuna njia nyingi ambazo wakulima wanaweza kupata pesa kutokana na ufugaji wa ng’ombe wa maziwa.

Unaweza kutengeneza pesa kutokana na kuuza samadi, ndama wako, na muhimu kabisa uzalizaji wa maziwa mengi.
Kuwekeza kwenye ng’ombe wa maziwa kwanza unahitaji kuorodhesha gharama zote utakazokumbana nazo.

Hizi ni pamoja na :

  • Banda la ng’ombe
  • Vifaa vya kukamulia maziwa
  • Lishe: Unaweza kupanda malisho kama Calliandra na Napier kwenye shamba lako.
  •  Madini ya kuongeza
  • Daktari wa mifugo na ada za madawa.

Bei ya ng’ombe mwenye kutarajia ndama itategemea na kumbukumbu ya kuzalisha na maziwa. Mara tu ng’ombe anapopata  ndama na kuanza kukama maziwa, unaanza kutengeneza pesa. Kwa mfano, kama ng’ombe wako anatoa wastani wa lita 20 kwa siku, unaweza kuuza lita moja kwa KSH 40 na kupata KSH 800 kwa siku.
Unaweza kuwekeza kwenye vyakula vya ziada/visismuzi ili kusaidia kuongeza uzalishaji wako wa maziwa na kupata faida zaidi.
Hata hivyo, kabla ya kuanza biashara yako ya maziwa, hakikisha unakuwa na mpango wa biashara. Mpango mzuri wa biashara utakuonyesha malengo unayotaka kufanikisha na namna unavyopanga kuyafikia. Kwa kuongezea utakuwezesha kujua soko lako.

Lazima pia uweke kumbukumbu nzuri za ufugaji wako, maziwa na mahesabu ya uendeshaji wa biashara yako. Hii itakuwezesha kufatilia kama unatengeneza faida ama la.

Malisho

Kutengeneza maziwa mengi mazuri, ng’ombe wa maziwa wanahitaji lishe bora ya aina tofauti, ikiambatana na nguvu, mchanganyiko wa kiwango, protini, vitamin na madini.

Nguvu

Malisho mabichi

Malisho mabichi hususani huwa nia mjani kama vile nyasi za NapierLucerne na majani ya viazi vitamu na mengineyo.

Hivi huwa vina maji mengi.

  • Usilishe nyasi zilizotoka tu kukatwa kwa ng’ombe wako. Kata majani mabichi na uyaache sehemu yenye giza kufifia, kisha kata kata vipande vya inchi 2 ( 5cm) ili kumrahisishia ng’ombe wako kula. Hii haitapoteza malisho.
  • Ng’ombe wa maziwa anatakiwa kupewa kilo 15-20 za majani mabichi kwa siku, inapendekezwa kwa awamu mbili kwa mfano.moja asubuhi na nyingine jioni.

Malisho makavu

Malisho yanajumuisha vitu kama Mabua ya nganiMabua ya mpungaMabua ya mahindi na mazao mengine ya mboga mboga

Malisho makavu

  • upande wa mabua na pia kiwango kibaya.
  • Changanya sehemu moja ya malisho mabichi na sehemu moja ya malisho makavu kwa mfano gunia 1 la nyazi za Napier zilizokatwa katwa na gunia 1 la mabua ya ngano yaliyokatwa katwa.

Protini na chakula cha ziada

Dania

Dania ni chanzo kizuri cha protini. Ng’ombe wako wanatumia protini kwaajili ya kujenga mwili na kuzalisha maziwa mengi ya kiwango bora.

Kilo 5 za Dania kwa siku ni protini ya kutosha kwa ng’ombe wako. Kama ng’ombe wako hawezi kupata protini ya kutosha kutoka kwenye malisho, tumia chakula cha ziada kama Kupakula kutoka Cooper-K Brands.

Chakula cha ng’ombe wa maziwa

Chakula cha ng’ombe wa maziwa kitampa ng’ombe vitamin, nguvu na protini katika njia ya uwiano, ili ng’ombe aweze kuzalisha maziwa mazuri na kuwa na uzito wa mwili wenye afya. Unga Farm Care (EA) wanapendekeza kulisha ng’ombe wako kilo 1 ya Fugo Dairy Meal kwa kila lita 2 za maziwa ng’ombe anazokupatia zaidi ya lita 5 za kwanza.
Hivyo, kama ng’ombe wako anakupa lita 7 kwa siku: 7-5 =kilo 1 ya dairy meal


Kwa ng’ombe wanaotoa lita 5 – 10 za maziwa kwa siku, wape gramu 400 za Kupakula. Mpe nusu asubuhi na nusu jioni. Kwa ng’ombe wanaotoa zaidi ya lita 10, ongeza gramu 400 kwa siku kila kwa lita 5 zaidi za maziwa juu ya lita 10. Hivyo kwaajili ya lita 20 , mpe kilo 1.2 kwa siku.

Vitamini na Madini

Kumpa ng’ombe wako madini kutafanya biashara yako ya ng’ombe wa maziwa kuwa nzuri. Ng’ombe wako atapata joto siku 60 baada ya kupata ndama hivyo utapata ndama ndani ya mwaka. Madini pia ni mazuri kwaajili ya uzalishaji wa maziwa na hali ya mwili. Madini ya poda, kama Maclik Plus na Maclik Super kutoka Cooper- K Brands ni mazuri kwaajili ya ng’ombe wakubwa. Changanya madini na chakula.

Maclik Plus

Kwaajili ya mtamba na ng’ombe aliekausha mwenye mimbaMpe gramu 10 ( ½ glasi) ya Maclik Plus kila siku.

Maclik Super

Kwaajili ya ng’ombe anaekamuliwa

Mpe gramu 200( glasi 1 ) ya Maclik Super kila siku.

Panda malisho mazao yako ya malisho kama Dania na Nyasi za Napier. Tumia samadi kutoka kwa ng’ombe wako kama mbolea.

Maji mengi

Maziwa yanatumia maji mengi. Unahitaji kuwapa ng’ombe wako maji safi mengi kila siku. Toa maji kwenye chombo cha maji kila baada ya siku 3 na weka maji safi

Share Now

Related posts