1. SIKU 1. Baada ya vifaranga kutotoleshwa ndani ya siku moja wapewe glucose kwa muda wa masaa mawili. Glucose huchanganywa katika maji na kupewa vifaranga hawa na baada ya hapo vifaranga wapewe mchanganyiko wa vitamins mfano ni AMINOVIT na OTC plus. Pia hii huchanganywa na maji. Vifaranga wawekwe katika eneo lenye joto wastani na safi. Baada ya hapo siku ya pili na kuendelea vifaranga wapewe. 2. SIKU YA 7. vifaranga wapatiwe chanjo ya NEWCASTLE (KIDERI). chanjo hii huchanganywa na maji safi katika eneo lenye kivuli kIsha kupewa vifaranga kwa muda wa…
Category: Utoaji Chanjo
SABABU ZA CHANJO KUSHINDWA KUMLINDA MNYAMA (KUFANYA KAZI). I Mshindo Media new
Ushawahi kujiuliza Ama kusikia mtu akisema, “ Mbona nimechanja na Kuku wangu bado wakaugua na Kufa!”Ama Mganga/Daktari analaumiwa “Mbona Mbwa/paka wangu ameugua na Chanjo ulitoa?” Kabla ya kupata hayo majibu tujiulize kwanza CHANJO ni NINI? Chanjo ni maandalizi ya kibailojia ambayo hutoa kingamwili(ulinzi) dhidi ya ugonjwa fulani, Kinga hiyo huwa ya Muda fulani au Maisha yote. Chanjo kwa kawaida ni vijidudu(Antigen) hai ama mfu ambavyo vinavyosababisha ugonjwa huo ila huwa Vimefubaishwa ili kutokuleta madhara katika mwili na hutolewa katika kiwango ambacho huweza kuamsha kinga ya mwili dhidi ya ugonjwa husika.Mfano.…
Magonjwa yanayo tibika kwa chanjo/Viral Infections (new)
Tujifunze Ugonjwa Wa Kuku Unaosababishwa Na VirusiGumboro (Ugonjwa wa Kuambukiza wa Bursar)* Ni ugonjwa unaosababishwa na virusi ambao hushambulia zaidi kuku, bata maji na bata mzinga. Kuku na bata wadogo hadi wiki 12 ndio wanaoathirika zaidi. Jinsi Ugonjwa Unavyoenea •Chanzo cha maambukizi ni maji, chakula na vifaa/vyombo vya shambani vilivyochafuliwa na kinyesi cha kuku wagonjwa na wenye vimelea. •Maambukizi pia huenea kupitia mfumo wa hewa, kwa vumbi lenye vimelea katika mabanda. Chukua Tahadhari Wageni, wafanyakazi na magari yanaweza kusambaza ugonjwa kutoka shamba hadi shamba au banda hadi banda. Hii ni…
RATIBA ZA CHANJO KWA KUKU TOKA VIFARANGA (new) I Mshindo Media
RATIBA ZA UTOAJI CHANJO Wakati wa kutayarisha mpango wa kuchanja kuku kwa ajili ya kinga dhidi ya magonjwa, kuna vipengele vikuu sita Ambavyo unatakiwa uvifahamu na kuvizingatia. Vipengele hivyo ni kama ifuatavyo: 1. Vifaranga vinavyoanguliwa kwa pamoja: Iwapo una kundi zaidi ya moja la vifaranga wanaoanguliwa, Weka utaratibu wa chanjo ambao utapunguza uwezekano wa magonjwa kuenea shambani. Hivyo basi, Hakikisha vifaranga na kuku wote wanapata chanjo kwa pamoja. 2. Umri wa kuchanja kuku: Kwa kuku ambao wanatarajiwa kutaga mayai au kuwa kuku wazazi, chanjo nyingi hutolewa si zaidi ya mwezi…
Usafi wa mabanda ya kuku na magonjwa ya virus (new)
DAWA MABANDA KABLA YA KUINGIZA KUKU· Ondoa mbolea na vitu vyote vilivyotumika(mifuko ya chakula,makopo n.k) na kuitupa mbali kabisa na mabanda· Anza kusafisha dari harafu kuta na kumalizia na sakafu· Lowesha vyombo vya kunyweshea maji na kulishia chakula na vifaa vyote vinavyotumika ndani ya mabanda kwenye dawa aina ya virutec kwa muda wa nusu saa harafu suuza na maji ya kawaida kabla ya kupiga dawa ya kuulia wadudu warukao na watambaao ndani nan je ya banda Kumbuka; Kuweka virutec kwenye footbath mlangoni kabla ya kuleta vifaranga Magonjwa yamegawanyika katika makundi mawili…
Fahamu kuku wa nyama na mayai (new)
SIFA ZA KUKU BORA WA MAYAI NA NYAMAKuku waliotunzwa vizuri tegemea yafuatayo:- Vifo wakati wa kulea 3% – 5% Vifo wakati wa utagaji 1% kwa mwezi Umri wa kuanza kutaga wiki 19-20 UTARATIBU WA CHANJORudia chanjo ya New Castle kila baada ya miezi 3-4, chanjo ya Mareks hufanyika Hatchery kabla ya mfugaji kupewa vifaranga.KUMBUKA:Chanjo ya mareks unaponunua vifaranga ni vigumu kujua,unatakiwa kuzingatia kupata vifaranga sehemu zinazotambulikaUTARATIBU WA CHAKULAUmri (Wiki) Aina ya chakula0-3 Broiler Starter4-8 Broiler FinisherTIBA YA MINYOOHii hufanyika zaidi kwenye kuku wa mayai:Mara ya kwanza wapewe wiki ya 8 kurudiwa ya 18Baada ya…
CHANJO KUSHINDWA KUMLINDA MNYAMA (KUFANYA KAZI (new) I Mshindo Media
Ushawahi kujiuliza Ama kusikia mtu akisema, “ Mbona nimechanja na Kuku wangu bado wakaugua na Kufa!”Ama Mganga/Daktari analaumiwa “Mbona Mbwa/paka wangu ameugua na Chanjo ulitoa?” Kabla ya kupata hayo majibu tujiulize kwanza CHANJO ni NINI? Chanjo ni maandalizi ya kibailojia ambayo hutoa kingamwili(ulinzi) dhidi ya ugonjwa fulani, Kinga hiyo huwa ya Muda fulani au Maisha yote. Chanjo kwa kawaida ni vijidudu(Antigen) hai ama mfu ambavyo vinavyosababisha ugonjwa huo ila huwa Vimefubaishwa ili kutokuleta madhara katika mwili na hutolewa katika kiwango ambacho huweza kuamsha kinga ya mwili dhidi ya ugonjwa husika.Mfano.…
Umuhimu wa Chanjo kwa Mifugo (new) I Mshindo Media.
Umuhimu wa Utoaji Chanjo kwa Mifugo: Tiba au kinga kwa chanjo iligunduliwa na mwanasayansi mwingereza, Bw. Edward Jenner ambaye katika karne ya 18 aligundua kwamba wahudumu wa ng’ombe katika maeneo fulani hawakupatwa na ugonjwa wa ndui (Small pox) kwa vile ng’ombe hao walikuwa na ugonjwa wa ndui ya ng’ombe (Cowpox).– Chanjo siyo dawa kama antibiotic, sulphonamate na kadhalika, bali ni ‘’mkorogo’’ maalum wenye vijidudu (microorganisms) ambavyo husababisha ugonjwa husika, lakini vimepunguzwa ukali wake kusudi visilete madhara kwa mtu au mnyama aliyechanjwa.– Chanjo husababisha mwili wa mnyama kuandaa ’’askari’’ waitwao antibodies…