Magonjwa yanayo tibika kwa chanjo/Viral Infections (new)

Tujifunze Ugonjwa Wa Kuku Unaosababishwa Na VirusiGumboro (Ugonjwa wa Kuambukiza wa Bursar)*

Ni ugonjwa unaosababishwa na virusi ambao hushambulia zaidi kuku, bata maji na bata mzinga. Kuku na bata 

wadogo hadi wiki 12 ndio wanaoathirika zaidi.

Jinsi Ugonjwa Unavyoenea

•Chanzo cha maambukizi ni maji, chakula na vifaa/vyombo vya shambani vilivyochafuliwa na kinyesi cha

kuku wagonjwa na wenye vimelea. 

•Maambukizi pia huenea kupitia mfumo wa hewa, kwa vumbi lenye vimelea katika mabanda.

Chukua Tahadhari

Wageni, wafanyakazi na magari yanaweza kusambaza ugonjwa kutoka shamba

hadi shamba au banda hadi banda. 

Hii ni pamoja na kuku hai, vifaa/vyombo vya shambani na bidhaa 

zitokanazo na kuku (mayai, nyama, manyoya na mbolea) wanaosafirishwa kutoka mashamba/mabanda 

yenye ugonjwa

Dalili

•Uharo mweupe wenye maji maji.

 •Kuku wanadonoana kwenye sehemu ya kupitishia haja, na sehemu hii huvimba.

•Kuku hulala kifudifudi.

 •Kuku wanashindwa kutembea na wanatetemeka.

•Vifo vya kuku vinaweza kufikia hadi asilimia 90, na kupungua kadiri ya siku.Fika

 •Hakuna tiba maalum

 •Kuku wapewe vitamini na antibayotiki na maji kwa wingi.

•Antibiotiki husaidia maambukizi nyemelezi. 

•Pata ushauri wa mtaalamu wa Mifugo.

Kuzuia

 •Kuku wagonjwa watengwe na walio wazima.

•Mizoga, makapi na vifaa vingine vilivyochafuliwa na kuku wagonjwa vichomwe moto au kuzikwa.

•Weka utaratibu madhubuti wa kupuliza dawa za viuatilifu vinavyofaa.

•Baada ya kumaliza kuwauza kuku wote, fanya usafi wa mabanda na kupuliza dawa.

Kinga/Chanjo

•Kuku, bata mzinga wapewe chanjo wakiwa na umri wa siku 14  na irudiwe tena wakiwa na umri wa siku 28 

 Chanjo ya Gumboro hutolewa mara 2 tu mpaka Kuku atakapo chinjwa au kuuzwa…………………………………………… …….

Share Now

Related posts