UTOTOLESHAJI WA MAYAI (new) I Mshindo Media

Kuna malalamiko makubwa sana kutoka kwa wafugaji kwenda kwa wauzaji wa mayai ya kutotolesha hasa kuhusu mayai kuto kutotoleshwa kwa kiwango kinacho tarajiwa. 
 Zijue sababu kuu za mayai kushindwa kutotolesheka 

👉👈 Yai kuto kurutubishwa, iwapo tetea atataga yai bila kupandwa na jogoo ni kwa 100% yai halita totolesheka 

 Suluhu Weka jogoo kwa uwiano huu unaoshauriwa Tetea 8-10 kwa jogoo mmoja na uhakikishe jogoo anapanda tetea. 

👉 👈 Hair line cracks (nyufa zisizo onekana kwa macho kwenye yai 

👆Kwa kawaida kuku hutaga mayai yenye ganda gumu, hivo iwapo mayai yatagongana sana wakati kuku wakitaga linaweza lisipasuke ila linaweka nyufa za ndani ambazo utaziona tu iwapo ni mzoefu wa kuchambua mayai (eggs sorting) au Kwa kumulika kwa tochi gizani. 

👆 Visababishi vya cracks hizi zisizo onekana 
👉Kuwa na idadi ndogo ya viota kuwianisha na idadi ya kuku inashauriwa kiota kimoja kichukue kuku 4-5 

👉Kuto weka randa au pumba za mpunga kwenye kiota anapotaga kuku, hivo yai likitagwa litagonga sakafu , bati au mbao na kuweka nyufa 

 Suluhu Weka randa au pumba za mpunga kwenye kiota cha kuku na ubadilishe kila baada ha wiki mbili. 

 👉Kuchelewa kuokota mayai na kufanya kwenye kiota kimoja kuwa na zaidi ya mayai 4 hii inatoa mwanya kwa mayai kugongana na kusababisha nyufa za ndani.

 Suluhu Nashauri kwa yeyote uwe mfugaji mkubwa au mdogo weka ratiba ya kukusanya mayai mfano 

Round ya 1 : SAA 1 na nusu asubuhi, 
Raundi ya 2: SAA 3 na nusu asubuhi 
Raudi ya 3: SAA 4 na nusu asubuhi 
Raundi ya 4: SAA 5 na 45 kisha nenda kula 
Raudi ya 5: Saa 8 mchana 
Raudi ya 6: SAA kumi nanusu jioni 

 Hapo cracks hautazisikia tena au zitapungua kwa asilimia kubwa shambani 

👉 Wakati wa kusafirisha mayai 
Hakikisha mayai yamepangwa kwenye tray na kuwekwa kwenye box gumu kuzuia ulegevu utakao pelekea mayai kugongana. 👏👏👏 

👉👈Tatizo la machine za kutotoleshe, hapa zingatia sana 
Temperature ( joto ) 
Humidity (unyevu ) 
Zinatia kadri mashine unayo itumia ilivo elekeza kwenye manual guide (mwongozo wa kutumia machine). 

👉👈 Mayai kukaa sana tangu siku ya kutagwa mpaka kuwekwa kwenye machine. 
Kitaalamu mayai yanayo wekwa kwenye machine yanashauriwa kukaa kwenye chumba maalumu chenye ubaridi *(Cold room yenye nyuzi joto 16-20°c kwa muda usio zidi siku 7 kisha yawekwe kwenye machine ) 

Ila kwakua wafugaji wengi hatuna hiki chumba maalumu cha kuhifadhi mayai kwenye joto sahihi, imekua ikishauriwa mayai kwaajili ya kuweka kwenye machine yasizidi siku 4 sababu kubwa ni moja tu 

👍Mayai yaliyo rutubishwa( yenye mbegu) yakikutana na joto huanza kutengeneza kifaranga hivo kama yai litabaki muda mrefu kabla ya kuwekwa kwenye mashine, ukija kuweka kwenye joto kubwa la incubator inatokea yule kifaranga alie anza kujijenga atakufa mapema *(early death)*  zingatia sana hii. 

👉👈Mayai kugeuzwa wakati wa kuweka kwenye machine( hii haizuii kutotoleshwa ila husababisha vifo vingi kwa vifaranga kabla ya kutotolewa) 

 Suluhu  Hakikisha ncha Kali imegeukia chini na Ncha butu iwe upande wa juu ( air sac iwe kwa juu ) kusaidia kifaranga kupata hewa ndani ya yai. 

SOMO HILI NI MAHUSUSI KWA 
#mfugaji muuza mayai ya kutotolesha 
#mtotoleshaji wa vifaranga 

NB : Watotoleshaji hakikisheni mnaset mayai masafi kwenye mashine kuepusha mrundikano wa bacteria unao pelekea maambukizi kwa vifaranga mnao wauza. 

Baada ya kutotolesha ( Hatching) Hakikisha umesafisha vema mazingira yako kwa strong Disinfectants kama 
VIROCID ili kuua asilimia kubwa ya vimelea

………………………………………..

Share Now

Related posts