Nguruwe: Magonjwa Yanayoshambulia Nguruwe na Tiba Zake

Magonjwa yanayoshambulia nguruwe yana tiba pia ni mengi kama ilivyo kwa wanyama wengine yanavyotokea lakini kuna magonjwa katika ufugaji wa nguruwe lazima uyajue pamoja na tiba zake kwakua ndio yanayo jitokeza mara kwa mara

ANAPHRODISIAS

Pale nguruwe anaposhindwa kuingia kwenye joto.hapa nguruwe anakua haingii kwenye joto hii inaweza kusababishwa Na uzito mdogo kutokana na kuwalisha chakula kisicho tosha au kisicho na virutubisho, uzito ulio zidi, upungufu wa madini, minyoo kwenye utumbo, magonjwa sugu.


LEPTOSPIROSIS

Dalili ya ugonjwa huu ni homa, kuhara,kukojoa damu na kupolomosha mimba kwa hatua ya mwisho na unaweza kuwatibu kwa streptomycin kabla ya tendo. Na unaweza kutumia dawa za antibiotic..

BRUCELLOSIS

Ugonjwa huu unatokea kwa dume na jike na inakua na dalili kama vile kunyonyoka manyoya,homa,kupooza miguu,kilema,na kutoa mimba mapema, na kwamjike ambao tayari wanazaa huzaa watoto zaifu,uke hua na mwekundu na pia kondo hutoka nje na kwa dume  hua na uvimbe kwenye mapumu ya nguruwe.Na ugonjwa huu hauna tiba hivyo chinja nguruwe wenye ugonjwa huu.


UTERINE PROLAPSE

Ugonjwa huu usababisha uterus kutoka nje,napia ugonjwa huu hauna tiba hivyo mnyama hutakiwa kuchinjwa..

MASTITIS

Bacterial husababisha kuvimba kwa kiwele na kupelekea kubadili uzalishaji wa maziwa,Dalili za ugonjwa huu ni kiwele kuvimba kua chamoto na maumivu napia uzalishaji wa maziwa upungua.Unaweza kutibu kwa kukanda chuchu ambazo na usiruhusu watoto kunyonya,toa maziwa yote kwenye kiwele baada ya hayo tumia antibiotics.penicillin-streptomycin..

ATROPHIC RHINITIS (KUVIMBA KWA PUA

Dalili ya ugonjwa huu kwa watoto wanakua wana koroma,kukohoa na kupumilia mdomo na unaweza kutibu kwa kutumia antibiotics na usafi pia ni muhimu


GREASY PIG DISEASE

Huu ni ugonjwa unao sababisha mabaka,vibarango kwenye ngozi,pia mnyama upungua kilo na anaweza kufa.zuia kwa kuzuia  ugomvi wa nguruwe kwa kuwakata meno,kuwapa chakula cha kutosha,usafi na tumia antibiotics

FOOT AND MOUTH DISEASE (FMD)

Huu ni moja ya magonjwa ya nguruwe Ugonjwa huu huathiri midomo na miguu ya nguruwe Ni ugonjwa ambao hushambulia nguruwe mara kwa mara hasa wasipokuwa na matunzo mazuri Ugonjwa wa miguu na midomo, hudhoofisha nguruwe kwa haraka sana, ikiwa ni pamoja na kupungua uzito.

Chanjo: Chanjo yake huitwa FMD VACCINATION nautolewa kila baada ya mwaka mmoja

Dalili: dalili zake miguu na midomo ya nguruwe inabadilika na pia nguruwe anadhoofika

Tiba: Ugonjwa huu hauna tiba halisi Inapotokea nguruwe wakawa wameshambuliwa kinachofanyika ni kutibu magonjwa nyemelezi kwa kutumia antibiotics.

huu ni ugonjwa wa mdomo na miguu na inadhulu wanyama wenye kwato

Dalili zake nguruwe anaweza kua kilema,homa na vidonda mdomoni na miguuniunaweza kutibu kwa kutumia antibiotics.Vaccination Disinfection No therapy (treatment)

ANTHRAX/kimeta

Huu ni moja ya magonjwa ya nguruwe unaosababishwa na bakteria wanaojulikana kama Bacillus anthracis, wadudu hawa wanabaki kuwa hai kwa muda mrefu na wanaweza kuwa kwenye udongo wakiwa hai kwa kipindi cha miaka mingi

Tiba: Unaweza kutibu nguruwe wako kwa kutumia dawa aina ya Penisilin au Oxytetracycline.

 Kimeta kinasababishwa na kuwalisha nyama nguruwe na

dalili zake ni

  • kupumua kwa shida,
  • kuvimba shingon,
  • homa na
  • kutoa kinyesi chenye damu

na mnyama alie kufa na kimeta hutoa damu maeneo ya wazi mwilini.

Na unaweza kutibu Kwa kutumia antibiotics.

2. Ugonjwa WA homa ya nguruwe

Ugonjwa huu unasambaa kwa kasi kama mmoja akiambukizwa wengine pia wataambukizwa na kufa

Dalili: nguruwe anakua na vidonda na vitu kama vibarango mwili mzima pia mdomo na masikio yanabadilika rangi nakua mekundu.

Chanjo: Ugonjwa huu hauna chanjo wala tiba. Kinachofanyika mlipuko unapotokea ili kuwa salama ni kuwateketeza nguruwe wote walioathirika na kuanza upya. Unaweza kuteketeza kwa kuwachoma moto.

Muhimu: Baada ya kuwateketeza nguruwe wagonjwa, safisha banda kisha nyunyiza dawa aiana ya Acon au Ectomin, na uache banda wazi kwa kipindi cha wiki moja kabla ya kuweka nguruwe wengine kwa kua huu ni viral  disease

3. Ugonjwa wa mapafu kwa nguruwe

Huu ni moja ya magonjwa ya nguruwe ambayo Ushambulia sehemu za koo na mapafu ya nguruwe, Ugonjwa huu husababishwa na bacteria (Secondary bacterial), joto kupita kiasi, vumbi na gesi inayotokana na madawa makali.

Dalili: nguruwe hukooa na kupumua kwa shida sana

Tiba: Homa ya mapafu kwa nguruwe inatibika kwa kutumia antibiotics Pamoja na kuwaweka wanyama sehemu safi, isiyo na baridi kali au joto la kupitiliza kiwango.

………………………………………………………………………………………………….

Share Now

Related posts