Viral Infections/Gumboro (Infectious Bursar Disease) I Mshindo Media.

 (Infectious Bursar Disease)

Ni ugonjwa unaosababishwa na virusi ambao hushambulia zaidi kuku, bata maji na bata mzinga. Kuku na bata
wadogo hadi wiki 12 ndio wanaoathirika zaidi.

Jinsi Ugonjwa Unavyoenea.
•Chanzo cha maambukizi ni maji, chakula na vifaa/vyombo vya shambani vilivyochafuliwa na kinyesi cha
kuku wagonjwa na wenye vimelea.
•Maambukizi pia huenea kupitia mfumo wa hewa, kwa vumbi lenye vimelea katika mabanda.

Chukua Tahadhari.
Wageni, wafanyakazi na magari yanaweza kusambaza ugonjwa kutoka shamba
hadi shamba au banda hadi banda.

Hii ni pamoja na kuku hai, vifaa/vyombo vya shambani na bidhaa
zitokanazo na kuku (mayai, nyama, manyoya na mbolea) wanaosafirishwa kutoka mashamba/mabanda
yenye ugonjwa

Dalili.

•Uharo mweupe wenye maji maji.
 •Kuku wanadonoana kwenye sehemu ya kupitishia haja, na sehemu hii huvimba.

•Kuku hulala kifudifudi.
 •Kuku wanashindwa kutembea na wanatetemeka.

•Vifo vya kuku vinaweza kufikia hadi asilimia 90, na kupungua kadiri ya siku.

Tiba.
 •Hakuna tiba maalum
 •Kuku wapewe vitamini na antibayotiki na maji kwa wingi.

•Antibiotiki husaidia maambukizi nyemelezi.

•Pata ushauri wa mtaalamu wa Mifugo.

Kuzuia.
 •Kuku wagonjwa watengwe na walio wazima.

•Mizoga, makapi na vifaa vingine vilivyochafuliwa na kuku wagonjwa vichomwe moto au kuzikwa.

•Weka utaratibu madhubuti wa kupuliza dawa za viuatilifu vinavyofaa.

•Baada ya kumaliza kuwauza kuku wote, fanya usafi wa mabanda na kupuliza dawa.

Kinga/Chanjo.
•Kuku, bata mzinga wapewe chanjo wakiwa na umri wa siku 14  na irudiwe tena wakiwa na umri wa siku 28.
 Chanjo ya Gumboro hutolewa mara 2 tu mpaka Kuku atakapo chinjwa au kuuzwa.

Share Now

Related posts