#UFAHAMU UGONJWA WA MAFUA YA KUKU
Ni ugonjwa unaoitwa infectious coryza huenezwa na
bacteria. anaeitwa (hemophilus paragallinarum).
Ugonjwa huu hushambulia kuku aina zote. Na usipo kuwa
makini kwenye usafi wa banda na vyombo , kuruhusu watu kuingia ovyo bandani au kuku wa jirani kuja kuingia
kwenye banda lako; ugonjwa huu unaweza shambulia kuku wako kwa kila wiki.
#DALILI ZA UGONJWA HUU
_Kuvimba uso chini na nyuma ya macho.
_Kupumua kwa shida na kukoroma
_Kutoka makamasi puani,
_ Mdomoni kuwa na hali ya mterezo
_Macho kuvimba
_Kushindwa kula.
_Kupiga chafya , macho kuonekana kama yanatoka
machozi
#JINSI UGONJWA UNAVYOENEA
_Ugonjwa huu huenea kutokana kuku mmoja kwenda kwa
kuku mwingine, au kutoka banda moja kwenda banda
lingine.
_Chanzo cha maambukizi ni maji na chakula kilicho
chafuliwa na kinyesi cha kuku Mgonjwa.
_Ugonjwa huu uneea na kuambukizwa kwa mfumo wa
hewa pale kuku wanapopiga chafya.
Pindi ugonjwa unapo ingia bandani kwako wale kuku
watakao onesha dalili za ugonjwa huu , watenge kisha
wape tiba kuku wako wote; unatakiwa kuwatenga kwa ajili
ya kupunguza maambukizi bandani.
#DALILI ZA MZOGA UKIUPASUA
Usaha mweupe hadi njano huonekana kwenye macho na
ndani ya pua
Zipo dawa nyingi za kutibu ugonjwa huu antibiotic/ sulfa.
Hizi ni baadhi tu.
Fluban
Flutan
Ganadexil
Tylodox
Teramycin.
Trimazine nk
Tumia fluban,flutan kwa Kuku wanaooneshadalili za mafua bila vifo.
Tumia Ganadexil,tylodox kwa Kuku wenye mafua ambao
kuna vifo vingi
…………………………………………………………………………………………………………………………….