Kideri ni ugonjwa wa namna gani?
Ugonjwa wa Kideri (ama wengine huuita Mdondo) ni ugonjwa wa ndege wenye kuambukiza kwa kasi,ambao huathiri jamii nyingi za ndege wafugwao kama kuku, kanga na ndege wengine.
Ugonjwa wa Kideri unaweza kuua kundi lote la ndege uliowafuga ikiwa hawajachanjwa dhidi ya ugonjwa huo na ukitokea mlipuko wa ugonjwa huo, unaweza kuteketeza kuku wote kijijini mwako na hata vijiji vya jirani. Kwa hivyo, ni muhimu kuchanja kundi lako la
ndege/kuku!
Dalili za ugonjwa wa Kideri hutofautiana kutegemeana na:
Aina ya virusi
Aina ya ndege/kuku
Umri na afya ya ndege/kuku
Hali ya mazingira
Eneo gani la mwili lilikoshambuliwa na virusi vya kideri.
Kutokana na sababu zilizoorodheshwa hapo juu, hakuna dalili mahsusi za ugonjwa wa Kideri, lakini kuna dalili ambazo unaweza kuzitazama ikiwa una shaka kuwa kuku wako wanaugua ugonjwa wa Kideri:
Vifo vya ghaa bila kuonesha dalili zozote
Kuvimba kwa kichwa na shingo
Kuharisha uharo wa kijani
Utagaji wa mayai kushuka kwa kiasi kikubwa au kusimama kabisa
Kutetemeka, kichwa kugeuzwa upande mmoja,
Kupooza kwa mabawa na miguu
Vifo vingi katika kipindi kifupi
Hata hivyo, inapotokekea muda unagundua dalili hizo, unakuwa tayari umeshachelewa mno! Ndio maana inashauriwa
kuchanja ndege/kuku wako kila mara.
Ugonjwa wa Kiderihueneaje?
Ugonjwa wa Kideri huambukizwa kwa kiwango kikubwa mno na huenea kwa kukuwengine kwa kasi kubwa ndani ya muda
mfupi sana. Ugonjwa huenezwa kwa njia ya kinyesi na hewa. Unaweza kuenea pia kupitia:
Maji ya kunywa yaliyobeba virusi
Kugusa chakula kilichobeba virusi
Kugusa kuku wagonjwa
Kugusa vitu au mazao yaliyobeba virusi na kuku wagonjwa (nyama ya kuku, matumbo, mayai na manyoya)
Kugusana na watu au vyombo kutoka katika maeneo yaliyoathiriwa na ugonjwa (viatu, nguo, na matairi ya gari, ambavyo vyote vinaweza kubeba virusi vya ugonjwa)
Nyumba za kuku zenye virusi
Kuzuia ugonjwa wa Kideri kwa njia ya chanjo
Kuchanja kuku wako dhidi ya ugonjwa wa Kideri ndio njia bora ya kuzuia kuku/ndege wako wasipate ugonjwa huo. Iwapo kuku/ndege hawajachanjwa, wanaweza kuugua ugonjwa wa Kideri. Ikiwa wataugua ugonjwa huo, hawawezi kutibiwa au kupona.
Utachanjaje kuku/ndege wako dhidi ya ugonjwa wa Kideri
Pata chanjo kutoka wakala mzuri. Chanjo inayopendekezwa ni Chanjo ya Kideri I-2 (I-2 Newcastle vaccine). Kuna wazalishaji wengi wa Chanjo ya Kideri I-2 wakitumia majina mbalimbali ya kibiashara, lakini nimuhimu kuthibitisha kuwa unachonunua
ni chanjo ya I-2.
-Kamata kuku kwa uthabiti hukuukiwaegemeza upande
-Weka tone moja la chanjo ya I-2 kwenye jicho moja ikiwa unawachanja kupitia machoni.
-Dondoshea tone moja jichoni na subiri kuku achezeshe kope AU dondoshea tone moja puani na msubiri kuku avute hewa.
Kumbuka!
Chanja kila baada ya miezi mitatu kwa
kuku wa umri WOTE.
Chanja kuku wenye afya tuu. Chanjo si
kwa ajili ya kutibu au kuponyesha.
Epuka kuweka chanjo katika mazingira ya
kiwango cha juu cha joto na jua la moja
kwa moja
Chanjo ya Kideri I-2 (I-2 Newcastle
vaccine) huwalinda kuku dhidi ya
ugonjwa wa Kideri pekee
Lisha kuku wako vizuri
Iweke nyumba ya kuku katika hali ya usafina bila vijidudu daima. Nyumba inatakiwa kuwa na hewa ya kutosha na ikiwa imeinuliwa ili kinyesi na taka zingine ziweze kudondoka kwenye udongo pasipo kuchafua chakula au maji.
Weka eneo lenye dawa ya kuchovya miguu mlangoni pa nyumba ya kuku ili kuua vijidudu na virusi miguuni mwako kila mara uingiapo
Weka nyumba ya kuku mbali na zile za binadamu na wanyama wengine ili kuzuia kuenea kwa magonjwa
Safisha vyombo vya kulishia kuku na kunyweshea kwa kutumia maji vuguvugu yenye sabuni na badilisha chakula na maji kila siku.
Njia nyingine za kudhibiti ugonjwa wa Kideri
Iwapo kuku wako wameshaugua ugonjwa: Chinja kuku wako wagonjwa wote mapema iwezekanavyo. Inashauriwa kuchoma kuku wako wagonjwa na waliokufa hadi wawe majivu kabisa au kuzika kuku waliokufa, manyoya na matumbo yao katika kina kirefu cha udongo.
Usiuze au kuwapa watu kuku wagonjwa, kwani kitendo hicho kinaeneza ugonjwa
Usichanje iwapo kijijini kwako tayari kuna mlipuko wa ugonjwa wa Kideri. Hadi hapo kuku wa mwisho akifa kwa ugonjwa, subiri angalau mwezi mmoja kabla kuleta kuku wapya.
Punguza kukutana kwa kuku, bata, njiwa, na kanga
Kwa kuku wenye afya, walishe pumba za mahindi, mbegu za nafaka, majani,wadudu na minyoo. Hii itasaidia kuku kuwa na afya bora na kukua haraka.
Tafadhali muone asa mifugo au wasaidizi wa afya ya mifugo mara unapobaini dalili za ugonjwa au kupungua kwa uzalishaji wa mayai.