Kuna malalamiko makubwa sana kutoka kwa wafugaji kwenda kwa wauzaji wa mayai ya kutotolesha hasa kuhusu mayai kuto kutotoleshwa kwa kiwango kinacho tarajiwa.
Yai kuto kurutubishwa, iwapo tetea atataga yai bila kupandwa na jogoo ni kwa 100% yai halita totolesheka
Weka jogoo kwa uwiano huu unaoshauriwa Tetea 8-10 kwa jogoo mmoja na uhakikishe jogoo anapanda tetea.
Hair line cracks (nyufa zisizo onekana kwa macho kwenye yai
Kwa kawaida kuku hutaga mayai yenye ganda gumu, hivo iwapo mayai yatagongana sana wakati kuku wakitaga linaweza lisipasuke ila linaweka nyufa za ndani ambazo utaziona tu iwapo ni mzoefu wa kuchambua mayai (eggs sorting) au Kwa kumulika kwa tochi gizani.
Visababishi vya cracks hizi zisizo onekana
Kuwa na idadi ndogo ya viota kuwianisha na idadi ya kuku inashauriwa kiota kimoja kichukue kuku 4-5
Kuto weka randa au pumba za mpunga kwenye kiota anapotaga kuku, hivo yai likitagwa litagonga sakafu , bati au mbao na kuweka nyufa
Suluhu Weka randa au pumba za mpunga kwenye kiota cha kuku na ubadilishe kila baada ha wiki mbili.
Kuchelewa kuokota mayai na kufanya kwenye kiota kimoja kuwa na zaidi ya mayai 4 hii inatoa mwanya kwa mayai kugongana na kusababisha nyufa za ndani.
Suluhu Nashauri kwa yeyote uwe mfugaji mkubwa au mdogo weka ratiba ya kukusanya mayai mfano
Round ya 1 : SAA 1 na nusu asubuhi,
Raundi ya 2: SAA 3 na nusu asubuhi
Raudi ya 3: SAA 4 na nusu asubuhi
Raundi ya 4: SAA 5 na 45 kisha nenda kula
Raudi ya 5: Saa 8 mchana
Raudi ya 6: SAA kumi nanusu jioni
Hapo cracks hautazisikia tena au zitapungua kwa asilimia kubwa shambani
Wakati wa kusafirisha mayai
Hakikisha mayai yamepangwa kwenye tray na kuwekwa kwenye box gumu kuzuia ulegevu utakao pelekea mayai kugongana.
Tatizo la machine za kutotoleshe, hapa zingatia sana
Temperature ( joto )
Humidity (unyevu )
Zingatia kadri mashine unayo itumia ilivo elekeza kwenye manual guide (mwongozo wa kutumia machine).
Mayai kukaa sana tangu siku ya kutagwa mpaka kuwekwa kwenye machine.
Kitaalamu mayai yanayo wekwa kwenye machine yanashauriwa kukaa kwenye chumba maalumu chenye ubaridi *(Cold room yenye nyuzi joto 16-20°c kwa muda usio zidi siku 7 kisha yawekwe kwenye machine )
Ila kwakua wafugaji wengi hatuna hiki chumba maalumu cha kuhifadhi mayai kwenye joto sahihi, imekua ikishauriwa mayai kwaajili ya kuweka kwenye machine yasizidi siku 4 sababu kubwa ni moja tu
Mayai yaliyo rutubishwa( yenye mbegu) yakikutana na joto huanza kutengeneza kifaranga hivo kama yai litabaki muda mrefu kabla ya kuwekwa kwenye mashine, ukija kuweka kwenye joto kubwa la incubator inatokea yule kifaranga alie anza kujijenga atakufa mapema *(early death)* zingatia sana hii.
Mayai kugeuzwa wakati wa kuweka kwenye machine( hii haizuii kutotoleshwa ila husababisha vifo vingi kwa vifaranga kabla ya kutotolewa)
Zingatia:
Hakikisha ncha Kali imegeukia chini na Ncha butu iwe upande wa juu ( air sac iwe kwa juu ) kusaidia kifaranga kupata hewa ndani ya yai.
NB : Watotoleshaji hakikisheni mnaset mayai masafi kwenye mashine kuepusha mrundikano wa bacteria unao pelekea maambukizi kwa vifaranga mnao wauza.
Baada ya kutotolesha ( Hatching) Hakikisha umesafisha vema mazingira yako kwa strong Disinfectants ili kuua asilimia kubwa ya vimelea
……………………………………………………………………………..