Azolla Production
JIFUNZE KUZALISHA AZOLLA KWAAJILI YA MIFUGO YAKO
Unaweza tazama video hiyo apo juu.….
FAHAMU AZOLLA
Azolla ni aina ya blue green algae ambayo huweza kulimwa na kustawi vizuri katika mabwawa,mito, madimbwi na mitaro inayotuhamisha maji kwa muda mrefu kazi yake kubwa hufyonza nitrogen kutoka kwenye hewa pia hukua haraka sana katika maji yaliyotuama
Faida za Azolla
1. Hutumika kuongeza nitrogen kwenye udongo kwa kutumika katika utengenezaji wa mbolea vunde au kuyafanya kama matandazo shambani
2. Hutumika kama chakula cha mifugo kwasababu ina kiwango kikubwa cha protein 25%-30% hutumiwa na ng’ombe, mbuzi, kuku, nguruwe
3. Huongeza uzalishaji wa maziwa kwa ng’ombe asilimia 15-20
4. Pia hutumika kama tiba ya maji kwani huweza kuyafanya yaweze kutumika kwa muda mrefu inawafaa wale wenye mabwawa ya umwagiliaji
5. Huwasaidia wakulima na wafugaji kupunguza gharama za mbolea na chakula cha mifugo yao
5.Huongeza kipato/faida kwa wafugaji na wakulima
Kilimo cha AZOLLA katika eneo dogo la square mita 18 kina futi 1.5 ambapo unaweza kuvuna AZOLLA ya kula Kuku 100 kila siku.
MAHITAJI
1. Mbolea ya ng’ombe kilo 27-30
2. Maji
3. Udongo
4. Mbegu ya AZOLLA (culture) kilo 3
5. Mbolea ya kiwandani (single/tripple super phosphate) gram 90-100.
HATUA ZA KUFUATA KTK UPANDAJI
1. Andaa bwawa lenye ukubwa wa square mita 18 kina futi 1.5
2. Jaza udongo kwenye bwawa lako kwa kina cha 10cm
3. Weka Mbolea ya ng’ombe kwa kuisambaza juu ya udongo kilo 27-30
4. Weka Mbolea ya super phosphate kwakuirusharusha bwawani ili isambae juu ya Mbolea na udongo.
5. Jaza maji kwenye bwawa lako kufikia kina cha 10-15cm kutoka juu ya udongo,samadi na Mbolea
6. Ondoa leya itakayokuwa imetanda juu baada ya kumimina maji, kisha acha bwawa litulie kwa muda wa masaa 12-24.
7. Panda AZOLLA yako kwa kumimina bwawani(3kg).
8. Weka kivuli juu ya bwawa lako ili kuzuia mionzi ya jua kupiga moja kwa moja bwawani(direct sunlight).
9. Subiri kuvuna baada ya siku 15 kwa Mara ya kwanza baada ya hapo utakuwa ukivuna kila baada ya siku 2-3 kwa zaidi ya mwaka.
UTUNZAJI WA BWAWA
1. Ongeza Mbolea ya super phosphate kila wiki gm 90
2. Hakikisha bwawa lako haliishiwi maji
3. Kivuli kisipungue kwenye bwawa lako.
Asanteni kwakusoma maandishi haya, ELIMU HAINA MWISHO penye mapungufu karibu tuboreshe ili tuweze kupunguza gharama za chakula cha mifugo yetu.
ZINGATIA: Si kila AZOLLA inafaa kulishia mifugo zipo zilizofanyiwa utafiti.
NAMNA YA ULISHAJI
Chakula cha Azolla unaweza ukawapatia mifugo kwa namna mbili.
1. unaweza ukawapatia kwa kuchanganya na vyakula vingine kwa kuweka azolla kilo 50, pumba kilo 25, na kilo 25 za chakula cha madukani/ ulichochanganya mwenyewe ili kupata kilo 100
2: unaweza ukawapatia Chakula cha Azolla tu bila chakula kingine, na hii hufanyika kwa Kuku wanauchunga hasa wa kienyeji.
…………………………………………………………………………………………………………………………..