CHAKULA CHA VIFARANGA WA KIENYEJI (new) I Mshindo Media

JINSI YA KUCHANGANYA CHAKULA CHA VIFARANGA  WA KIENYEJI  

MIEZI MIWILI YA MWANZO.

Unga wa dona wa nafaka kama mahindi au mtama 40kg

Pumba za mtama au mahindi au uwele 27kg

Mashudu ya alizeti au ufuta, au pamba au karanga n.k. 20kg

Unga wa mifupa au chokaa ya kuku (DCP) 2.25kg

Dagaa au mabaki ya samaki (sangara fish meal) 10kg

Chumvi ya jikoni 0.5

Virutubisho (Broiler premix) 0.25

JUMLA = 100kgs.

Huu mchanganyiko ni wa vifaranga kuanzia siku 1 hadi miezi miwili.

JINSI YA KUCHANGANYA CHAKULA CHA KUKU WA KIENYEJI, . WA  MIEZI 3 MPAKA WA 4.

Mahindi yaliyobarazwa au mtama au uwele 25

Pumba za mtama au mahindi au uwele 44

Mashudu ya alizeti au ufuta, au pamba au karanga n.k. 17

Unga wa mifupa au chokaa ya kuku (DCP) 3.25

Dagaa au mabaki ya samaki (fish meal) 10

Chumvi ya jikoni 0.25

Virutubisho (Broiler premix) 0.5.

JUMLA = 100Kg

JINSI YA KUCHANGANYA CHAKULA CHA KUKU WA KIENYEJI WA  MIEZI 5 MPAKA WA 6. (Hadi kuuzwa) 

Mahindi yaliyobarazwa au mtama au uwele 31

Pumba za mtama au mahindi au uwele 38

Mashudu ya alizeti au ufuta, au pamba au karanga n.k. 18

Unga wa mifupa au chokaa ya kuku (DCP) 2.25

Dagaa au mabaki ya samaki (fish meal) 13

Chumvi ya jikoni 0.5

Virutubisho (Broiler premix) 0.25

JUMLA = 100 kgs

NB: mchanganyiko huu ni kwa ajili ya kuku wa biashara hu mfanya kuku awe na mafuta. Ila kama kuku wako unataka badae waje watage katika mchanganyiko huo utawapa mwisho kwenye mwezi wa Tatu.

Kuanzia mwezi wa nne utawapa mchanganyiko huu hapa chini ili kuwa andaa kwa ajili ya kutaga

KWA KUKU KIENYEJI WANAO TAGA. 

Dagaa  2 kg

Damu   2 kg

Alizeti    8 kg

Pumba ya mahindi   5 kg

Mahindi yalio barazwa    24 kg

Chokaa    5 kg

Mifupa    4 kg

Layers premix gm  150

Methionine gm  50

Chumvi  gm 30

Naamini umeongeza maarifa katika mpangilio wetu wa vyakula kwa ajili ya kunenepesha kuku kiasilia.

Share Now

Related posts