SIFA ZA KUKU BORA WA MAYAI NA NYAMA
Kuku waliotunzwa vizuri tegemea yafuatayo:-
Vifo wakati wa kulea 3% – 5%
Vifo wakati wa utagaji 1% kwa mwezi
Umri wa kuanza kutaga wiki 19-20
UTARATIBU WA CHANJO
Rudia chanjo ya New Castle kila baada ya miezi 3-4, chanjo ya Mareks hufanyika Hatchery kabla ya mfugaji kupewa vifaranga.
KUMBUKA:Chanjo ya mareks unaponunua vifaranga ni vigumu kujua,unatakiwa kuzingatia kupata vifaranga sehemu zinazotambulika
UTARATIBU WA CHAKULA
Umri (Wiki) Aina ya chakula
0-3 Broiler Starter
4-8 Broiler Finisher
TIBA YA MINYOO
Hii hufanyika zaidi kwenye kuku wa mayai:
Mara ya kwanza wapewe wiki ya 8 kurudiwa ya 18
Baada ya wiki 18 wasipewe tena na dawa ya minyoo hadi baada ya kufikia kiwango cha juu cha utagaji (peak production)
Baada ya Peak Production kuku wapewe dawa ya minyoo kila baada ya wiki 8-10 au minyoo inapoonekana kwenye kinyesi
KUKU WA NYAMA (BROILERS)
Kila kuku wa nyama anapaswa apate eneo la futi moja (1) ya mraba. Nyumba iwe na madirisha ya kutosha, hewa safi, sakafu iwe na godoro (litter) ya randa au maganda ya mpunga.
VIFAA
Vifaranga 100 wanaweza kutumia chombo kimoja cha kulishia (chick plate) na chombo kimoja cha kunywea maji (chick fount) kwa wiki moja kuanzia wiki ya pili na kuendelea tumia chombo kimoja cha kulishia (feeder) chenye kipenyo cha sentimenta 38 kwa kuku 50 .
Fuata ratiba ya chanjo kama ilivyopendekezwa
Pata chanjo toka sehemu inayojulikana na yenye uhakika wa upatikanaji
Hifadhi chanjo yako kwenye fridge na sio freezer sehemu yenye nyuzijoto 4 – 8 centigrade.
Chanjo isitolewe zaidi ya saa 4.30 asubuhi kwa sababu chanjo inaweza kuharibika kutokana na joto au mwanga mkali wa jua.
Unapoona dalili za ugonjwa, kama kusinzia, kujikunyata, kuharisha, kutokula chakula, kutokunywa maji, kuhema kwa tabu au vifo, toa taarifa haraka kwa mtaalamu wa mifugo ili upate ushauri na huduma mara moja.
……………………………………………………………………………………………………………….