Umuhimu wa Chanjo kwa Mifugo (new) I Mshindo Media.

Umuhimu wa Utoaji Chanjo kwa Mifugo:

Tiba au kinga kwa chanjo iligunduliwa na mwanasayansi mwingereza, Bw. Edward Jenner ambaye katika karne ya 18 aligundua kwamba wahudumu wa ng’ombe katika maeneo fulani hawakupatwa na ugonjwa wa ndui (Small pox) kwa vile ng’ombe hao walikuwa na ugonjwa wa ndui ya ng’ombe (Cowpox).
– Chanjo siyo dawa kama antibiotic, sulphonamate na kadhalika, bali ni ‘’mkorogo’’ maalum wenye vijidudu (microorganisms) ambavyo husababisha ugonjwa husika, lakini vimepunguzwa ukali wake kusudi visilete madhara kwa mtu au mnyama aliyechanjwa.
– Chanjo husababisha mwili wa mnyama kuandaa ’’askari’’ waitwao antibodies ambao pindi vijidudu hai vya aina hiyo vikiingia mwilini hukabiliana na askari hao.
– ‘’Askari’’ hao huweza kukaa mwilini mwa mnyama kwa muda maalum. Nguvu zake zikipungua inabidi chanjo itolewe tena. Wataalamu wanajua muda unaostahili kurudia chanjo, inaweza kuwa miezi mitatu, sita au mwaka.
– Chanjo huongeza uwezo wa mnyama wa kujikinga na magonjwa pamoja na kupunguza chembechembe nyeupe za damu ziitwazo ‘’leucocytes’’.

FAIDA ZA KUTOA CHANJO:
– Kuchanja ni njia ya uhakika ya kulinda afya ya mifugo.
– Chanjo hudhibiti magonjwa yasiyoweza kutibika.
– Chanjo hudhibiti magonjwa yanayosababishwa na virusi, pia kuna chanjo kwa ajili ya magonjwa yanayoletwa na bakteria:
– Chanjo hutumiwa zaidi kudhibiti magonjwa yafuatayo:
             – Sotoka ya ng’ombe (Rinderpest)
             – Kichaa cha mbwa. (Rabies)
             – Kideri ya kuku. (Newcastle).
             – Kimeta kwa ngombe (Anthrax)

MASHARTI YA UTOAJI CHANJO:
– Mfugaji lazima ahakikishe mifugo yenye afya nzuri ndiyo inayochanjwa
– Mtaalamu wa afya ya mifugo lazima ashirikishwe kwenye shughuli hii.
– Kuku hupata chanjo kwa ajili ya magonjwa yafuatayo:
                     – Ugonjwa wa Marek’s – Vifaranga siku ya kwanza.
                     – Ugonjwa wa Kideri – Vifaranga siku ya saba.
                     – Ugonjwa wa Gumboro – Vifaranga siku ya kumi na nne.
                     – Ugonjwa wa Ndui – Wenye umri wa miezi miwili.
Chanjo ni muhimu kwa mifugo ya jamii zote ili kuepuka uwezekano wa kuenea kwa magonjwa mbalimbali.
Chanjo kwa ng’ombe, mbuzi na kondoo
         – Ugonjwa wa miguu na midomo: Mara moja kila mwaka.
         – Ugonjwa wa kimeta: Mara moja kila mwaka.
         – Ugonjwa wa homa ya mapafu : Mara moja kila mwaka.
         – Homa ya bonde la ufa : Mara moja kila mwaka.
         – Homa inayoathiri farasi wa Kiafrika: Mara moja kila mwaka.

CHANJO KWA MBUZI 

MAFANIKIO YA UTOAJI CHANJO:
Chanjo inaweza kuleta matokeo yaliyokusudiwa ikiwa:
              – Chanjo haikai kwenye hali ya joto au mwanga wa jua.
              –  Mifugo ina afya bora kabla ya kuchanjwa
              – Huduma ya chanjo inatolewa na wataalamu wa kazi hii.
………………………………………………………………………………………………………………..

Share Now

Related posts