MAMBO YA KUZINGATIA KWA VIFARANGA SIKU 30 MPAKA 60 (new) I Mshindo Media

…………………………………..

🐓🐓🐓🐓🐓🐓🐓 

Yapo mambo muhimu ya kuzingatia siku  za mwanzo kwa vifaranga wako ili wakue vyema na kukuletea matokeo chanya. 

✔️ Banda liwe Safi na liwe linatosha kwa vifaranga kulingana na square meters pendekezwa.  Wasibanane kwani huweza kuleta ukuaji usio sawia na kupelekea vifaranga 

🐓 kudumaa .

🐓kudonoana hovyo .

🐓kulaliana .

🐓kuambukizana. magonjwa kirahisi. 

✔️Chakula kiwe bora na chenye virutubisho vyote muhimu kwa vifaranga kama vile protin, wanga, carbohydrates nk  

Pia kiwe na madini ya kutosha kama vile DCP, Chokaa, mifupa nk,  Epuka kujichanganyia Chakula kiholela kwani inaweza kupelekea 👇

🐓vifaranga kulemaa miguu na kushindwa kusimama kwa kupungukiwa madini mwilini 

🐓vifaranga kuvimba macho 

🐓 vifaranga kupata magonjwa yanayo shambulia mfumo wa Chakula Mara kwa Mara .

🐓 vifaranga kudumaa na kuchukua muda mrefu kukua. 

🐓kupungukiwa kinga za mwili yani *chick body* *immunity*. Na kupeleka kutosihimili magonjwa pindi yaingiapo bandani .

Vifaranga wanapokuwa na kinga ya kutosha mwilini husitahimili magonjwa kwa muda mrefu kabla ya kuleta vifo.  Hii humsaidia mfugaji kukabiliana na tatizo kwa muda kidogo. 

🐓vifaranga huota manyoya ambayo hayana mpangilio na muda mwingine huchelewa hata kuota manyoya jambo ambalo humlazim mfugaji kuendelea kutumia vyungu joto kwa muda mrefu. 👇👇

Vifaranga ni bora wapewe Chakula cha kiwandani ndani ya siku 30 mpaka 60 . Baada ya hapo unaweza kuchanganya Chakula mwenyewe ila kwa kutumia formula sahihi. 

✔️ Vyombo vya Chakula na maji viwe Safi muda wote.  Epuka kutumia Vyombo vinavyo vujisha maji kwani itapelekea Banda kuwa na unyevu muda mwingi na kusababisha Magonjwa. 

✔️ joto liwe sahihi na lipunguzwe kila wiki kwani kadiri vifaranga wanavyokuwa wakubwa ndivyo joto linazidi kutohitajika bandani.  Mara nyingi vyanzo joto huwa ni ndani ya siku 30 mpaka 36. 

✔️ Chanjo zitolewe kwa wakati na kwa Ratiba maalum.  Chunguza maendeleo ya vifaranga wako siku Tatu kabla ya Chanjo ili kubaini kama kuna ugonjwa wowote.  Kukiwa na mambukizi bandani usiwape vifaranga wako Chanjo mpaka pale utakapo watibu na kupona.  Kuku mgonjwa asipewe Chanjo mpaka apone kwanza .

✔️Matandazo yawe Safi muda wote 

✔️ Hewa iingie na kutoka bandani bila kuleta athari zozote 

✔️ Vifaranga wenye ulemavu watengwe 

✔️ Maji yawe hayana chumvi ya kiwango kikubwa cha kusababisha shida kwa vifaranga 

✔️ kama unatumia buruda ni vizur vifaranga watumie mpaka ifikapo wiki 8 na kupelekwa kwenye grower point wiki 9. 

✔️ Maji yenye kiwango kikubwa cha chlorine hayafai kwajili ya Chanjo kwani chlorine ni disinfectant hivyo hupunguza nguvu ya Chanjo kwa kuuwa bacteria hai /viruses ambao ndio tunawatarajia kutumika katika Chanjo. 

Fuata maelekezo ya kitaalam kabla ya kutumia maji hayo. 

🐓🐓🐓🐓🐓🐓👆👆

Hayo ni machache ya kuzingatia . Nitaendelea kubainisha menginge mengi kadiri muda unavyo ruhusu. 

🙏🙏🙏🙏🙏 niwatakie ufugaji mwema wenye tija

……………………………………………………………………………………..

Share Now

Related posts