MAFUNZO MBALI MBALI RAHISI NA HALISI KWA MFUGAJI
ULISHAJI
👉Lisha kuku muda mmoja kila siku, usibadilishe badilishe ratiba
👉Usibadilishe badilishe chakula
👉Usiwapunje wala kuzidisha chakula
👉Wawekee vyombo vya kutosha
👉Maji yawepo muda wote
👉Vyombo vya maji visafishwe kila siku
UOKOTAJI WA MAYAI
👉Panga ratiba maalumu ya kuokota mayai, mfn SAA 7:30/Am, saa 10:30 Am, saa 1:30 Pm, saa 4:30 Pm, funga report.
👉Safisha viota vya kuku, kuondoa vinyesi kila asubuhi na ongeza matandazo mayai yasipasuke
👉Okota mayai na yaweke kwenye Trey upande uliochongoka utazame chini, na upande butu uwe juu
👉Weka mayai sehemu salama isiyo na joto jingi
👉Mayai ya kutotolesha yahifadhiwe kwa siku zisizo zidi 10
UHIFADHI WA KUMBUKUMBU
👉Hakikisha umeweka kumbukumbu zote za msingi shambani kwako kama
👆Aina ya kuku
👉Siku ya kuingia bandani
👉Idadi yao na wanaokufa
👉Gharama za chakula
👉Gharama nyingine zote
👉Mauzo
🐣Piga hesabu mapato na matumizi, hii itakusaidia kujua na kutathmini kama mtaji unakupa faida au unajiendesha kwa hasara.
BIOSECURITY/VIUMBE HAI SALAMA
👉Usichanganye kuku na mifugo wengine
👉Usiruhusu kila mtu kuingia bandani
👉Mavazi maalumu na buti maalumu za bandani
👉Panya na ndege wazuiwe kuingia bandani uwezavyo
👉Kuku wachanjwe kwa wakati
👉Kuku waliokufa waondolewe bandani kwa wakati
JIONGEZE KITAALUMA
👉Wapeleke watunzaji kuku semina za ufugaji
👉Kama mmiliki hudhuria warsha na maonesho kujifunza ufugaji
👉Uwe mfuatiliaji wa mradi wako Mara kwa Mara
👉Ajiri /tafuta mtaalamu kuwa anaangalia mradi wako
👉Lipa vizuri wafanyakazi wako🐣
UPANUZI WA MRADI
👉Tafuta wateja wapya kila wiki
👉Imarisha uaminifu kwa wateja wazamani
👉Hakikisha bidhaa haiishi bandani, kama itaisha tafuta namna ya kumuwezesha mteja kupata bidhaa , ukikosea wanakimbia.
👉Panua mradi pindi gharama za uanzishaji zinapo rejea, usisubirie mpaka kuku wazeeke
MUHIMU
👉Ukihitaji uzalishaji bora usiogope kugharamia wataalamu
👉Pata miongozo tofauti ya ufugaji kupanua uelewa