ULEAJI WA VIFARANGA WA KIENYEJI KWA NJIA YA KISASA (new)

UFUGAJI WA KUKU

JINSI YA KUTUNZA VIFARANGA WIKI 1-5

Kuku ni ndege wafugwao na binadamu wengi kwa ajiliya matumizi mbalaimbali ya binadamu. Mara nyingi hutumika kwa ajili ya kitoweo na kwa biashara pia. Wafugaji wengi hupenda kufuga kuku maana ni mwepesi kumtunza na hana garama kubwa za utunzaji ukilinganisha na wanyama wengine wafugwao. leo tutaangali jinsi ya kuwalea vifaranga had wafae kuwa kuku wakubwa;

Nyumba ya vifaranga;

nyumba ya vifaranga inatakiwa kuwa karibu na nyumba ya kuishi ili uweze kuwaangalia vifaranga kwa ukaribu zaidi, ijengwe kwenye sehemu iliyotulia kulingana na mwelekeo wa upepo na kuta zisiingize baridi sana pia iwe na eneo la kutosha kulelea vifaranga.
  mfano wa nyumba ya vifaranga iliyotengenezwa na mfugaji mwenyewe

nyumba hiyo imejegwa maalumu kwa ajilinya kutunzia vifaranga katika ustadi mzuri kabisa.
Baadhi ya wafugaji hutengeneza nyumba za kufugi ilimradi katengeneza bila kutumia vipimo au ufanisi mzuri ili kulea vifanganga vizuri.
   mfano wa nyumba ya vifaranga ambayo haijatumia ufanisi wowote kulingana na taratibu na kanuni za kulea na kutunza vifarnga ;
vifaranga hutoka wakati wote na kuzurura hivyo ni hatari kwa wanyama wakali kama vicheche mwewe na wengine wanaoweza kuwadhuru vifaranga . ni vyema kutengeneza banda bora kwa ajili ya kufugia vifaranga kwa uangalifu mzuri kukwepa hasara.

  Vyombo kwenye nyumba ya vifaranga; 

       ni muhimu kuweka vifaa safi kwenye nyumba ya vifaranga kwa ajili ya kuwalishia na kuwalelea. kipo kitu kinaitwa kitalu hiki ni kwa ajili ya kutunzia vifaranga visitawanyike ndani ya banda. taa ya chemli, jiko la mkaa pia ni vifaa muhimu vya kulelea vifaranga pindi wawapo wadogo banadani bila kuwa na mama yao.

chanjo na tiba

vifaranga vinatakiwa kupewa chanjo kulingana na ratiba ya chanjo inavyotaka pindi tu wanapoanguliwa toka kwenye yai lake. wafugaji wengi hawapend kufuata utaratibu wa chanjo ndo maana wengi huambulia hasara pale magonjwa ya milipuko yanapotokea . ni vyema kumtumia mtaalamu kwa ajili ya maelekezo jinsi na kupata na kutumia chanjo kwa usahihi ili kukwepa kuingia hasara kwa matumizi mabaya ya dawa.
unapo ona tofauti kwenye kuku wako unashauriwa kutumia dawa mapema na kuwatenga fifaranga wote wenye dalili ya kuumwa ili kukwepa kuwaambukiza vifaranga wengine ndani ya banda lakoooo kama mfugaji.

………………………………………………………………………………………………………

Share Now

Related posts