UFUGAJI WA BROILERS/ KUKU WA NYAMA (new) I Mshindo Media

MWONGOZO WA UFUGAJI WA KUKU WA NYAMA/BROILERS 

Biashara ya kuku imejikita katika uwanja mpana sana kwa kutegemea aina za kuku, kwa maeneo mengi ya mjini Kuku wa nyama wamekua wakiuzika sana Japo kwa bei isiyo rafiki kwa mfugaji 

👉Kwa maeneo mengi wafugaji wamekua wakifuga wakitarajia kuuza kuku kuanzia siku ya 28-30, au kama watachelewa sana basi wasizidi siku 35, japo wapo wengine ambao huuza mapema zaidi ya hapo au kwa kuchelewa kutokana na sababu tofauti tofauti. 

👆Mambo ya kuzingatia ili broilers waweze kukua ipasavyo. 

👉 Chakula 
👆Kwa ukuaji wa haraka wa broiler anatakiwa kupewa chakula muda mwingi wa Siku, kutoka kwa wafugaji wazoefu wa broiler wametoa shuhuda kwamba broiler wawashiwe taa masaa 24 na wapewe maji na chakula. 

👏Kwa makadirio ya kuku 100, broilers wamekua wakitumia mifuko ya chakula kama ifuatavyo 
👉Broiler starter crumble siku 1-13 mfuko mmoja 

👉Broiler Grower Pellets siku 14-22 mifuko miwili 

👉Broiler finisher Pellets siku 23-kuuza mifuko miwili 

NB: Zipo shuhuda kwamba broiler 100 wanaweza kutumia mifuko minne pekee mpaka kuuza, hii inategemea sana aina ya vyakula na nafasi yao bandani. 

👆Wafugaji wengi wamekua mbali na kulisha chakula wanawapa vitamin , mollases na Booster kama ifuatavyo 
👉Neoxychick &multivitamin siku 1-5 
👉Vitamin kama Amintoto siku ya 7-10 
👉Bro-booster na Mollases siku ya 11-24 
👉Avipunch booster siku zilizo salia mpaka kuuza 

👉👈 Matumizi hayo ya vitamin sio sheria , kutumika ili kupunguza gharama. 

👆 CHANJO 
Kwa uzoefu wangu  mfumo ambao nimezoea kuutumia 
👉Siku ya 7 newcastle/kideri 
👉Siku ya 14 Gumboro 
👉Siku ya 21 Newcastle 

Mfumo B 
👉Newcastle siku ya 7 
👉Gumboro siku ya 14 
👉Gumboro siku ya 21 

NB: Ndui haichanjwi kwa broiler, ila kwa wakati mwingine wamekua wakipata ndui iwapo watachelewa kuuzwa 

NAFASI 
👆Kitaalamu broilers 10 wanafaa kukaa kwenye mita moja mraba, hii itasaidia sana kupunguza case za broiler kuchafuka kwa kulowesha maranda. 

👆Kiasili broiler wanakunywa sana maji, hii hupelekea banda kuloana sana, hali hii imepelekea wafugaji wengi kuwa na kawaida ya kubadilisha randa Mara kwa Mara 

👈Kubadili randa mara kwa Mara kwa mtazamo si sawa, ila unaweza ukawa unatoa palipo lowana sana na kubadilisha na randa kavu, hii itakusaidia sana kupunguza ugonjwa wa Mafua. 

👆👉Nashauri kama itakua lazima sana basi randa zibadilishwe Mara 3 pekee IKIBIDI 

👉👆👈 MASOKO 
👉Broiler wamekua wakiuzwa sana , kwa mtu mmoja mmoja, familia, supermarket, wauzaji wa nyama mitaani, mahoteli, mashule na sehemu kadha wa kadha NASHAURI tafuta soko lako la uhakika na uwe tayali kulilinda bei za broiler zinatofautiana mkoa kwa mkoa. 

👆👉👆 MFUMO WA UGUGAJI 
👉Ili kuhakikisha soko lako linakua lakudumu na kuepuka kupoteza wateja nashauri 

👆Kama una mtaji ya kuku 500, nivema ukaingiza kuku 250 wiki hili, kisha 250 baada ya wiki 2 hii itarahisisha mzunguko wa pesa ya mradi, USIFUGE  Kuku 500 kisha ukakaanao siku 30 ukiuza ndo uweke wengine itakua ngumu sana kukuza mradi (kutokana na research ndogo niliyofanya pindi nawatembelea wafugaji). 

👆Kama nyama nyingine nyeupe, broilers pia wanasaidia kuimarisha afya ya malaji, ila mfugaji jitahidi kuto tumia kiwango kikubwa cha madawa ambayo yanaweza yakamdhuru mtumiaji wa mwisho 

MAGONJWA KWA BROILER 
👉Coccidiosis, kuhara ugoro au damu (dawa Agracox, vetacoxy, au Anticox kwa wanaohara damu) 

👉Mafua , wahi mapema kubaini na unaweza kutumia ( Fluban, Flutan, Tylodox, na Enrovet) 

Dawa hizi unapowapa wape na vitamin kupunguza stress kwao 
……………………………………………………………………………

Share Now

Related posts