MWONGOZO WA KUKU WA MAYAI (new) I Mshindo Media

MWONGOZO WA KUKU WA MAYAI. 

👉Kuku wa mayai, hawa ni kuku ambao vinasaba vyao huwawezesha kutaga mayai mengi kwa muda watakao fugwa 

Zipo aina nyingi za kuku wa mayai hapa nitataja baadhi 

👆Hy-line, Isa brown, Bavon brown, Lohman brown, Rhode Island n.k 

Yapo mambo kadhaa ya kuzingatia kwa kuku wa mayai 

👏ENEO 
👉Idadi ya kuku kwa mita moja mraba ni kuku 7-8 ndio inayo shauriwa sana kitaalamu kwa ukuaji na kuzunguka 

👉Vyombo vya chakula na maji 

Belly drinker 1 kuku 60-80 

Chicken /feeder drinker kubwa Lita 20 kuku 50-60 

Chicken  drinker/feeder ndogo lita 10 kuku 20-25 

Hii huwezesha kuku kupata maji ya kutosha 

👉👈NB : Kuku anatakiwa kunywa maji zaidi ya Mara mbili ya chakula anachokula kwakua zaidi ya 75% ya yai ni maji, ukipunguza maji wanapunguza kutaga 
ZINGATIA 

👉Kuku wapewe chakula kwa ratiba sahihi iliyo zoeleka usibadilishe ratiba utawastress na wataounguza kutaga 

👉Mfano huwa unalisha saa 6 AM na 4 PM hakikisha unawalisha kila Siku muda huo 

👏Kuku walishwe kwa mfumo wa gramu ili kuzuia kujaza mafuta au kutumia chakula kingi kuzalisha yai moja, kwa kawaida kuku mmoja wa mayai anatakiwa kukupa mayai 6-7 kwa kilo 1 ya chakula (Hyline) 

Mfn: Unakuku 100, wiki ya 20, wanatakiwa kula gram 120 kwa kuku mmoja 
👉👈Chukua 120× 100=12000gram 
👆12000/1000=12 kg 
Kwahiyo kuku hao wiki hilo watakula Kilo 12 za chakula kwa siku. 

Kuku wana pitia stage 3 

Brooding wakiwa vifaranga mpaka wiki 4, 

Growing wiki 5 -17 na Production baada ya kuanza kutaga mayai 

Hivi vipindi vinatofautiana kiuangalizi na kipindi cha kutaga hutegemea vipindi hivi( Brooding au malezi ya vifaranga na Growing) 

Brooding zingatia 
Chakula, Joto, hewa safi, Mwanga, nafasi ya kukaa inashauriwa 40 chicks kwa 1m2( vifaranga 40-60 kwa mita 1 mraba) 

Growing 
Zingatia chakula, Mwanga , nafasi na Hewa safi kwakua hapa ndo kuku anakua anaandaa mfumo mzima wa mayai 

CHAKULA 

👉Starter kwa wiki1- 6/8 

👉Grower 7/8-17 au watakapo anza kutaga 

👉Layers mash baada ya kuokota yai nakuendelea,  hii huanza Mara nyingi wiki ya 18-20 ndipo kuku wengi huanza kutaga. 

👏👈Kuku wakianza kutaga nivema ukawapa masaa 16 ya Mwanga kama somo la mwanga linavoelekeza yaani ,mchana masaa 12 mwanga wajua ,kisha jioni unawasha taa na kuizima saa 4 usiku. 

Ratiba za chanjo 

👉Siku ya 7na 21 Newcastle (ya maji au matone) (LASOTA) 

👉Siku ya 14na 28 gumboro( Ya maji) 

👉Siku ya 30ndui(Ya bawa) 

👉Kila baada ya miezi 3 rudia chanjo ya Newcastle 

👉Wape dawa za minyoo kila baada ya miezi mitatu.mfn Piperazine, Levifarm, Fenbemdazole, (Mtafute Daktari wa mifugo) 

👆👇USHAURI 
👉Uza mayai na uweke akiba kwaajili ya kuingiza kuku wengine , tunashauri uingize kuku kwa kutofautisha rika hii itakusaidia kukuza mradi pia kuwawezesha wateja wako kupata huduma muda wote. 

👉Weka kumbukumbu ya gharama zote ulizotumia 

👉Chanjo za maji, ziwekwe kwa masaa mawili pekee, kisha badilisha maji na kuweka maji mengine (yanaweza kuwa na vitamin au maji matupu), ila watolee maji masaa 2 kabla ya kuwapa chanjo na uwape chakula kuongeza kiu, (inashauriwa kuchanja Asubuhi au jioni) 

👉Fuatilia kwa makini idadi ya vifo ,ili ujue kuku waliobaki kupima uzalishaji( usipokua makini utaibiwa) 

👉Epuka kutumia dawa bila kumshirikisha Daktari wa mifugo, dawa nyingine hupunguza au kukata utagaji mayai kwa muda , Zenye salfa kama Esb 3 n.k. 

👉Hakikisha randa bandani haziloani, kuepusha magonjwa ya Coccidiosis,  na ya kuumia miguu kwa kuunguzwa na Ammonia bandani. 

👉Fanya tathmini ya mradi Mara kwa Mara, angalau kila mwezi 

👉Jitahidi sana kutafuta taarifa za masoko mkoani kwako na mikoa mingine , kupanda, kushuka kwa soko ili uweze kuuza kwa bei zilizopo (Usiwe nyuma) 

👉Wahudumu wa kuku, wapate huduma zote za msingi kama wanao , usiweke GEP baina yao na familia , watapenda kazi na uzalishaji utakua mzuri na hawataiba ( Boresha maslahi) 

👉Zingatia sana sheria za Viumbe hai salama, BIOSECURITY kupunguza case za magonjwa 

👉👆 Kwa wanaofuga kwa cages. 
👉Huu ni mfumo mzuri na rahisi kwa kuku 
👆Mayai masafi 
👆Hayapasuki 
👆Wafanyakazi wachache 
👆Magonjwa hupungua 
👆Chakula hakimwagiki sana 

👉👆Inashauriwa kuku wawekwe kwenye cages wakifikisha umri wa wiki 12-14, kuzoea mazingira ili wasipate stress. 

👆👉👈 Madaktari, wataalamu na wafugaji wazoefu mwaweza ongeza ushauri pia tufikie malengo 
………………………………………………………………………..

Share Now

Related posts