MUHTASARI WA UFUGAJI KUKU I Mshindo Media (new)

1: Maandalizi ya banda la kuku, Fagia, deki kwa maji, pulizia dawa/disinfection (Th4, V rid,Farm guard nk). 

Acha banda likae zaidi ya siku 7 baada ya kutoa kuku wakubwa kabla ya kuingiza kuku wengine. 

Andaa vifaa vyote muhimu kwa ajili ya kupokea kuku wapya vikae bandani angalau siku 3 kabla ya kupokea vifaranga.

Andaa sehemu ya kulelea vifaranga, weka vyanzo vya joto tayari kabla vifaranga hawajafika(Usikurupuke kuweka wakati vifaranga wameshafika). 

2: Maandalizi ya chakula na maji 

Hakikisha maji, chakula kwaajili ya kuku wako yapo bandani au sehemu ya karibu muda wote ili kurahisisha ulishaji wa kuku. Chimba kisima au weka tank la kuhifadhia maji na uwe na stoo ya kuhifadhia chakula ( isiruhusu panya kuingia ) 

Hakikisha kuku wamepewa chakula muda sahihi na kwa kiwango sahihi kulingana na umri na aina ya kuku wako. 

3: Idadi ya kuku bandani. 

Ili kupelekea ukuaji murua wa kuku, zingatia nafasi sahihi (idadi sahihi ya kuku kwa mita 1 mraba) 

Mfano( Pure layers 7-8 kwa 1m², Chotara na kienyeji 3-4 kwa 1m², Broilers 10 kwa 1m²,) hii itakusaidia kutengeneza kuku wanao wiana uzito na maumbo VIFARANGA 40 kwa 1m². 

4: Idadi ya vyombo vya maji na chakula , 

Kwa kuzingatia aina ya na size ya vyombo unavyo tumia , hakikisha kuku wako wote wanapata nafasi sawa ya kula na maji 

 Mfano Vifaranga 60-70 kwa chicken drinker 1 kwa wiki ya kwanza kisha punguza mpaka idadi ya 45-50 kwa wiki mbili mbele. Sahani pana  za kulia vifaranga (1kwa vifaranga 60-80). 

 Kuku wakubwa 
Feeder 1 kubwa ya Lita 10 kwa kuku 20-25/30 

Drinker 1 ya lita 20 au Belly drinker kubwa kwa kuku 50-60 
NB Idadi ya vyombo vya maji na chakula izingatie kwamba kuku wote wanapata nafasi ya kula wakati wa kulisha wasiwepo wanaozunguka kwa kukosa nafasi. 

 RATIBA ZA CHANJO 

Kuku chotara, Pure wa mayai  tumia mwongozo huu kwa chanjo kuu zilizo zoeleka 

Siku ya 1 mareks 
Siku ya 7 Newcastle (Lasota) 
Siku ya 14 Gumboro 
Siku ya 21 Newcastle 
Siku ya 28 Gumboro 
Siku ya 30(wiki 4-5) Ndui inategemea ukanda ulipo 
Baada ya miezi mitatu rudia new castle. 

 BROILERS/KUKU WA NYAMA 
Siku ya 7 Newcastle 
Siku ya 14 Gumboro 
Siku ya 21 Newcastle au Gumboro) 
Hatuchaji ndui kwakua kuku wanauzwa mapema 

 Kwa kutegemea eneo lako imezoeleka kuchanja kwa mfumo upi 

 ULISHAJI 
Kuku wa nyama kwa mujibu wa mwongozo wangu Mimi KAHISE. 

Siku 1 hadi siku ya 13 Broilers Starter Crumble 
Siku ya 14 hadi 22 Broilers Grower Pellets 
Siku ya 23 mpaka kuuza Broilers Finisher Pellets 
 (Kuku wapewe vitamins)  Ratiba hii inatofautiana kutoka kwa mfugaji mmoja kwenda kwa mwingine chamuhimu kuku wafikishe 1.3-1.5 kg kwa siku 30 

 KUKU KWAAJILI YA KUTAGA 

Wiki 2 za kwanza (Broiler starter crumble) kuwakuza haraka na wawe na umbo kubwa mapema. 

Wiki ya 3 mpaka wiki 7-8 Chick starter Mash. 

Wiki ya 7-9 Layer Grower Mash mpaka watakapo dondosha yai lakwanza 

Layers mashi kutoka pale utakapo ona yai la kwanza ( kuanzia angalau wiki ya 18-20) kulingana na aina ya kuku mpaka utakapo amua kuwatoa bandani. 

NB Zingatia unapohama kutoka aina 1 yachakula kuingia aina nyingine CHANGANYA VYAKULA HIVYO KWA SIKU 3-4 ili kuwazoesha na kutowapa STRESS. 

Wape kuku walioanza kutaga jumla ya masaa 16 ya mwanga( Nyongeza ya masaa 4 ya mwanga wa taa) au zima taa usiku saa 4. 

…………………………………………………………………………………………………………………

Share Now

Related posts