MBINU KUMI ZA KUFUGA KUKU KWA MATOKEO BORA ZAIDI (new) I Mshindo Media

Habari za wakati huu ndugu msomaji wa makala zetu na mfugaji wa kuku.Ni imani yetu kuwa uko sawa kabisa na mradi wako unaenda kama ulivyotegemea.Kama mambo hayaendi sawa basi endelea kuwasiliana nasi tusaidiane kukabiliana na changamoto unazopitia na kushauriana zaidi.Leo tungependa kutoa elimu mujarabu juu mbinu  sahihi za kufuga kuku ili mfugaji aweze kupata matokeo mazuri katika ufugaji wake.

1. Mtaji; Kabla hujaamua aina ya kuku wa kufuga ni vema ukabaini hali yako kifedha. Maana kuku hutofautiana katika ufugaji kwa gharama zao. Hivyo ni lazima ukajua kiasi ulichonacho kulingana na kuku uwatakao kabla ya kuanza ufugaji. Si chini ya asilimia 70 zitatumika kununulia chakula . Ipo aina ya kuku wanao fugwa kwa gharama naafuu na kukupa matokeo kwa haraka kwa kuwa wanakaa bandani mda mfupi. Lakini pia ipo aina ya kuku ambao hufugwa kwa gharama kubwa sana na huleta matokeo kwa kukaa bandani baada ya mda mrefu.. mfano kuku wa nyama wanaanza kuuzwa wakiwa na umri wa wiki 4 . Na kuku wa mayai huanza kutaga wakiwa na umri wa miezi 5 ndipo uanze kupata faida.
2. Hakikisha una taarifa za uhakika za masoko; Upatikanaji wa masoko na taarifa zake ni jambo la msingi na muhimu na lamsingi kabisa kwa mfugaji ili uweze kupata thamani ya bidhaa yako kabla hujaamua ni aina gani ya kuku wa kufuga. Mfugaji fuatilia taarifa zake za soko kwa maeneo yaliyo jirani mawewe na kwa usahihi zaidi. Wengi wanafuga kuku ukifika muda wa kuingiza kuku sokoni ndipo tunaanza kuhangahika na masoko. Na matokeo yake tunashindwa kupata tija stahili kutokana na kuzalisha bidhaa zisizo endana na masoko na kupelekea kushindwa kufanya vizuri kwa kushindwa kufanya vizuri kimauzo kwa kuuza bidhaa bei ndogo na kutumia madalali kwani unakua na wasiwasi wa masoko. Nakushauri anza kidogokidogo na kwa masoko ya karibu yako. Mimi nina imani kila familia kuku
3. Aina ya kuku: Chagua aina ya kuku wenye uwezo wa kutaga mayai mengi na wakati huohuo, kuzalisha nyama nyingi. Hii itakupa faida kote, kwenye upande wa nyama na upande wa mayai. Kuku hawa wanajulikana kama Chotara, wanatabia sawa na kuku wa kienyeji wenye asili ya Tanzania wanaopatikana maeneo mengi nchini; kutokana na uvumilivu wao wa magonjwa na hali tofauti za mazingira. Pia wanauwezo wa kutaga mayai mengi (Wastani wa mayai matano kwa wiki) karibu sawa na kuku wa kizungu. Aina ya kuku hawa ni kama vile, Chotara wekundu (Rhode Island Red), Black Australorp (Weusi/Malawi), Barred Plymouth Rocks (Madoa), New Hamshire Red,Sasso na Kuroila .Hizi ni aina ya kuku zinazo patikana Tanzania.
4. Zingatia sana Chanjo: Kama nilivyosema mwanzo, kuku wa kienyeji ni wavumilivu wa magonjwa lakini si kwamba hawayapati, kuna magonjwa ambayo ni hatari pia kwa kuku wa kienyeji. Chanjo ni muhimu kuwaepusha na hatari ya kuyapata magonjwa haya. Chanjo muhimu kwa kuku wa kienyeji ni; New Castle, Gumboro, Marek’s na Ndui ya kuku. Fuata utaratibu wa chanjo kutokana na ushauri wa daktari. 
5. Chakula bora: Kuku wanahitaji mchanganyiko sahihi wa chakula, ili waweze kukupatia mazao mengi na bora, na kuwaepusha na magonjwa. Zipo fomula mbalimbali za chakula kutokana na umri wa kuku, na aina ya kuku. Kuku wote wanahitaji chakula chenye mchanganyiko sahihi wa Madini, Vitamini, Protini, Fats, Wanga, Vyakula vya kulinda mwili ili usipatwe na maradhi, na Maji safi. Muhimu kuwapatia kuku majani kama ziada ya chakula, hii hupunguza gharama za chakula na kuwafanya kuku waonekane wenye afya bora. Ni vizuri kuwapatia vifaranga chakula spesheli cha dukani kama huna ujuzi wa kutengeneza mwenyewe. Kwani vifaranga wengi hufa kutokana na kutokupata chakula chenye mchanganyiko sahihi kwao. Kuku wa mayai pia wanahitaji mchanganyiko sahihi ili waweze kutaga mayai kwa wingi.Ukihitaji kupata fomula ya kuchanganya chakjula cha kuku wa umri wowote usisite kuwasiliana nasi tutakupatia kwa bei rahisi sana.Fomula zetu ni zile ambazo tumezitumia kwa muda mwingi na zimekuwa na matokeo mazuri sana katika mradi wetu wa Africhick.
6. Banda liwe bora: Kuku wa kienyeji pia, wanahitaji banda au nyumba ya kuku imara ili kuweza kuwakinga na baridi kali, wanyama hatari, na wizi. Banda pia liwe na semu nzuri za kutagia na sehemu za kulala ziwe juu , kwani kuku hupendelea kulala juu. Ni muhimu banda liwe katika hali ya usafi muda wote. Kwa hivyo ni vizuri linyanyuliwe juu kidogo ili kuruhusu uchafu kuanguka chini na lijengwe ka kutumia mbao, mabanzi, milunda, nyavu, na mabati. Vifaranga wanahitaji kutenganishwa na kuku wakubwa. Banda si lazima liwe la gharama kubwa, kwani mafanikio ya ufugaji wa kuku ni vile unavyo waangalia na si banda. Mada inayohusu mabanda bora ya kuku imo katika kitabu chetu kinachofundisha mambo yote muhimu katika ufugaji wa kuku ambacho kipo mitamboni na kitatolewa muda si mrefu.Endelea kuwasiliana nasi kwa namba za simu au email kuweka oda yako sababu watakaoweka oda mapema watauziwa karibia nusu ya bei.
7. Zingatia uwiano wa Majogoo kwa mitetea : Ili mayai mengi yaweze kutotolewa, ni vizuri jogoo mmoja aweze kuwahudumia majike wasio zidi 7. Jambo ambalo wengi hatulijui ni kwamba,kuku wanaweza kutaga bila ya jogoo, lakini mayai hayatoweza kuleta kifaranga. Ili mayai yalete vifaranga ni lazima yawe yamerutubishwa (Fertilized eggs) na jogoo. Kwa hivyo ni vizuri kuweka Jogoo 1 kwa majike 7, hivyohivyo Jogoo 2 majike 14, Jogoo 3 majike 21, n.k. Pia hakikisha kuku wanao tumika kuendeleza kizazi ni wale wenye afya bora.Ukitaka kuwachagua mitetea ya kuatamia,hakikisha unachagua wale wenye manyonya mengi(maumbo makubwa),hii itasaidia mayai yote yaweze kupata joto stahiki. 
8. Vyombo vya chakula na maji : Hakikisha vyombo vya chakula na maji ni visafi na vinawatosheleza kuku wote. Vyombo hivi ni vizuri vifanyiwe usafi wa mara kwa mara, ili kuwaepusha kuku na magonjwa. Maji machafu huwa ni chanzo kikuu cha magonjwa hasa ya kuhara. Hakikisha kuku wako wanabadilishiwa maji angalau mara mbili au moja kwa siku pale utakapo ona maji yamechafuka.Sio bussara hata kidogo banda la kuku kukaa bila maji ya kunywa.Chakula kuku anapimiwa lakini kuku ni sharti awe na maji wakati wote awapo bandani.
9. Kuwa tayari kwa tiba ya kuku wakati wote: Kufuga kibiashara inategemea upambane na changamoto za magonjwa ya kuku katika mazingira yako,magonjwa hutegemea ukanda unaofugia kuku,mfano kuna magonjwa ambayo hushamili katika ukanda fulani kama vile mdondo/kideri. Ndui ya Kuku na gumboro.Magonjwa yamegawanyika katika makundi makuu mawili
A.Magonjwa yanayohitaji chanjo-kama vile mdondo/kideri,ndui ya kuku,Mahepe(mareck),Gumboro.magonjwa haya hayana dawa za kuyatibu zaidi hupewa dawa za kupunguza athari tuu.
B.Magonjwa yanayotibika kwa dawa- kama vile kuhara damu,homa ya matumbo,mafua ya kuku na Wadudu kama vile minyoo na Viroboto,utitiri na chawa.hivyo ili ufanikiwe katika ufugaji wako yakupasa uwe tayari kwa matumizi ya dawa pale yatakapohitajika.
Kuku hasa wa chotara ama kisasa akiugua haitamchukua mud asana kuwaambukiza wengine bandani.Unashauriwa kuwa na record ya magonjwa yanayotokea mara kwa mara na kujiandaa kwa fedha ama madawa ili kuweza kukabiliana na changamoto za magonjwa wakato wowote.Jambo la msingi unalotakiwa pia kuelewa hapa ni kuwa,hakikisha kila siku unatenga muda wa kukagua kuku wako kwa kuingia bandani na kuwatazama kama wamechangamka,kama wanakula na aina ya rangi ya kinyesi chao.Ukiona hali yoyote isiyo ya kawaida wasiliana na mtaalamu akupe suluhisho.Ukipenda pia unaweza kujiunga na group letu la ufugaji wa kuku ambalo linawasaidia sana wafugaji wakiwa na changamoto yoyote inayohusiana na kuku.Ili kuwa na wanachama ambao wako commited, tumeweka kiingilio kidogo sana na uzuri ni kwamba ukishaingia katika group hakuna gharama za ziada,wewe ni kufaidi tu.Wasilian na namba za simu unazoziona hapa chini uweze kuungansihwa katika group.
10. Tafuta mtu aliye wahi kufanya utakacho kifanya na akafanikiwa .Katika kila jambo lifanywalo na mwanadamu bila shaka uzoefu ndio jambo la msingi kuliko yote katika kulifanikisha jambo hilo uzoefu huweza kusaidia hata uharaka wa utatuzi wa haraka changamoto.
Maana mara nyingi changamoto utakazo kabiliana zinakuwa ni zilezile zinazo jirudia lakini kufanya kwa kutumia muda mrefu sio sababu pekee ya kufanikiwa kwenye unacho taka kufanya. Hivyo ni wajibu wetu kujifunza kila kukicha.Shughuli ya ufugaji ni shughuli ambayo inapaswa ifanywe kwa uangalifu mkubwa mno unao zingatia kanuni na taratibu zake. Hivyo kujifunza kutoka kwa wengine ni jambo lisilo epukika kwa mfugaji ambaye kweli anataka kufanya shughuli ya ufugaji na kuiweka kama shughuli itakayo kuwa inamwingizia kipato chako cha kutosha. Usisite kugalamia semina au mafunzo yoyote zitolewazo na watu mbalimbali maana kupitia semina ndimo watu wanamo jifunzia. Usiogope kutoa kiingilio jiulize unacho pata ni sawa na hela yako uliyo to.Mfugaji huna budi kuwa mbunifu kwa kila kitu unanayo pitia ufugaji. Ubunifu unatakiwa kuzingatiwa utendaji wa sgughuli zetu za kila siku. Kwanzia kwenye kutaga kuku hadi kwenye kuuza bidhaa zake. Ubunifu ninao maanisha ni ule ambao utakuwa umelenga kuboresha shughuli nzima za ufugaji na kukupa taswira chanya. Ubunifu ndio utakao kupa dhamani ya bidhaa yakoMfugaji kabla hujaanza kufuga ni vema ukafahamu vigezo vikuu vya kutaalamu vinavyo hitajika kwenye kila hatua ya ufugaji. Ni lazima ufahamu kwa makini zaidi kuku anavyo paswa kufugwa kwa kila hatua. Maana bidhaa nyingi zinazo zalishwa na wafugaji kiko chini ya kiwango kwakuwa kanuni hazizingatiwi ipasavyo. Maana utakuta mfugaji anafuga hata chanjo ya magonjwa hajui zaidi asubiri kuku aumwe ndipo amtibu.
Kama umefuatilia andiko letu kwa umakini utabaini kuwa mchakato wa ufugaji wa kuku bibiashara ni mchakato mpana ambao unahitaji mpango mathubuti,umakini lakini zaidi uwe na uelewa wa kutosha kuhusu kile unachokifanya.Ndio maana tumeamua kupunguza gharama za kujiunga nagroup letu Whatsap ili kuwa na wafugaji walio serious zaidi na wanaotaka kuufanya ufugaji kama ajira.Ukihitaji kujiunga nasi tumia nmaba zilizopo hapo chini tutakupa maelekezo.Tunaomba pia ieleweke pia,katika group letu hatuhitaji mizaha wala mambo yasiyohusiana na ufugaji wa kuku.Hivyo kama ukija na ukatoa kiingilio halafu ukaanza kuleta mambo ya sijui nguvu za kiume mara sijui fedha za freemason tutakuondoa mara moja.Ahsanteni na iweni na ufugaji mwema kwa maendeleo ya taifa letu.
…………………………………………………………………………………….

Share Now

Related posts