JINSI YA KULEA VIFARANGA VYA KUKU (new) I Mshindo media

JINSI YA KULEA VIFARANGA VYA KUKU

Karibu mpenzi msomaji wa MSHINDO MEDIA , leo hii napenda kuwaletea soma la jinsi ya kulea vifaranga vya kuku, hivyo tusiache kua nasi ili kujifunza mengi zaidi.

Na tutaanza na jinsi ya kujenga nyumba ya vifaranga, hivyo ukitaka kujenga nyumba ya vifaranga nilazima uzingatie yafuatayo.

Nyumba ya vifaranga nilazima ijengwe karibu na nyumba ya muangalizi hii ni kwaajiri ya kuweza kuwa karibu kwa uangalizi zaidi.

Nyumba ijengwe hatua 20 au zaidi mbali na nyumba ya kuku wakubwa hii nikwaajili ya kupunguza maambukizi ya magonjwa.

Nyumba ya vifaranga isiruhusu unyevu, baridi na wanyama au wadudu kuingia ndani, lakini ni lazima iwe na mwanga wakutosha

Pia nyumba ya vifaranga inatakiwa kua na uwazi wa kutosha kuwezesha vifaranga kutobanana na waweze kutembea kwa uhuru.

pia ijengwe eneo ambalo haliruhusu upepo kutoka kwenye nyumba ya kuku wakubwa kuingia hii itapunguza maambukizi ya magonjwa.

 JIFUNZE MIFUMO YA KUFUGA KUKU

UKUBWA WA NYUMBA

Ukubwa, vifaranga hawaitaji eneo kubwa katika wiki 4 za mwanzo, kwa makidirio mazuri mita squire moja huchukua vifaranga 16, na baada ya wiki 4 za mwanzo unatakiwa kuongeza eneo ili kuwapa nafasi zaidi.

Sakafu, sakafu inayo faa ni ile ya simenti ikichanganywa na zege au unaweza kuchukua kinyesi cha ng’ombe kilicho changanywa na maji kisha ukasiliba chini, unaweza kuchagua aina gani ya sakafu kati ya hizo kulingana na uwezo wako.

Ukuta, unaweza kujenga ukuta kwa kutumia matofari, bati, mabanzi au debe kulingana na uwezo wako, urefu unatakiwa kua futi 6-8 kutoka chini kwenda juu futi 3-4 za chini nilazima zizibwe na ukuta na futi 3-4 za juu unaweka wavu wa chuma au fito kulingana na uwezo wako, na ukuta ulio jengwa kwa tofari nilazima upigwe lipu.

Dirisha, madirisha yanaweza kuzibwa kwa kutumia mabokis au mkeka ikishwa wekwa nyavu, kulingana na uwezo wako.

Paa, Paa nilazima liwe zuri lisilo vuja na unaweza kuweka tundu la kutoa hewa y joto 

Nitumaini langu umepata elimu ya kutosha na usisite kua nasi ili kuendelea kupata elimu zaidi.

……………………………………………………………………………………………………………………………………..

Share Now

Related posts