Kaya nyingi hapa nchini hujihusisha na ufugaji wa kuku kwa lengo la kujipatia chakula na kipato. Mazao yatokanayo na ufugaji wa kuku ni pamoja na mayai, nyama, mbolea na manyoya kwa ajili ya matumizi mbalimbali. Mifumo ya ufugaji kuku ambayo hutumika hapa nchini ni huria, nusu huria na shadidi. Ufugaji wa kuku utakuwa endelevu na wenye tija kwa kufuata kanuni za ufugaji bora zifuatazo:- • Kufuga kuku kwenye banda bora • Kuchagua kuku bora wa kufuga • Kutunza na kulisha kuku kulingana na hatua mbalimbali za ukuaji • Kudhibiti na kutibu magonjwa ya kuku • Kutunza kumbukumbu BANDA LA KUKU Kuku huhitaji banda bora ili…