Ni ugonjwa unaowapata jamii ya ndege ambao unasababishwa na vimelea aina ya
paramyxovirus.
Kuenea kwa Ugonjwa
Ugonjwa wa Mdondo (Newcastle disease) huenea kupitia njia mbalimbali kama zifuatazo:-
- Mayai ya kuku aliyeugua ugonjwa wa mdondo/kideri (Newcastle disease).
- Kugusana na kuku mgonjwa.
- Kupitia maji yenye maambukizi.
- Wakati wa totoleshaji vifaranga.
- Chakula chenye maambukizi.
- Hewa yenye maambukizi ya ugonjwa huu.
Dalili za Mdondo/Kideri (Newcastle disease)
- Vifo vya ghafla.
![](https://animalscience.care/wp-content/uploads/2023/11/image.jpeg)
2. Kutoa udenda mdomoni.
![](https://animalscience.care/wp-content/uploads/2023/11/image-1.jpeg)
3. Kukosa hamu ya kula.
![](https://animalscience.care/wp-content/uploads/2023/11/image-3.jpeg)
4. Kuharisha kinyesi cheupe na kijani.
5. Kuhema kwa shida.
![](https://animalscience.care/wp-content/uploads/2023/11/image-2.jpeg)
6. Kukakamaa viungo au kupooza hasa mabawa, shingo na miguu.
7. Kupunguza utagaji.
8. Vifo hutegemea kasi ya ugonjwa huweza kufikia hadi asilimia mia moja (100%).
Namna ya kudhibiti Mdondo/Kideri (Newcastle disease)
![](https://animalscience.care/wp-content/uploads/2023/11/image-4.jpeg)
- Wapewe chanjo kwa muda unaofaa (Siku ya 7 na 28, na kila baada ya miezi 3).
- Kuku wote waliozidiwa (wagonjwa) wachinjwe na wafukiwe katika shimo lenye kina kirefu kuzuia kuenea ugonjwa.
- Fuata maelekezo ya Daktari au Mtaalam wa mifugo.
- Matibabu
- Hakuna matibabu ya ugonjwa huu, ila kwa msaada na ushauri zaidi katika ufugaji wasiliana na Daktari au Mtaalam wa mifugo.