Bila kupoteza muda banda lakuku linalofaa linatakiwa liwe na yafuatayo:-
- lizungushiwe kuta fupi ili liweza kuwakinga na upepo.
- liwekwe paa ili kuwakinga dhidi ya mvua.
- banda liwe na nafasi ya kutosha ili kuku waweze kutembeatembea,kunywa maji ,kula chakula,kutaga nk.
- sakafu iwe imara na isiyoruhusu unyevunyevu na harufu mbaya.
Banda liruhusu hewa ya kutosha kuingia na kutoka pia mwanga wa kutosha.
Kama umeezekea bati hakikisha pawe na miti karibu na banda ili irahisishe mzunguko wa hewa maana bati huchemka sana wakati wa mchana.
*Lisiruhusu jua kupenya ndani ya banda wakati wa mchana.waweza weka kuta ndefu za banda ziwe mashariki magharibi.
*weka majivu ndani ya banda au tumia dawa za kuua wadudu kama utitiri,siafu,utitiri waweza tumia Akheri powder,ultra vin,seven nk
*banda walau liwe na kuta fupi zenye kina cha mita 1.8
KUPUNGUZA MLIPUKO WA MAGONJWA
*Funika sakafu kwa maranda ya upana wa sentimita 5 na sambaza vizuri bandani.
Safisha mara kwa mara yanapochafuka.
*weka vichanja bandani ili kuruhusu kinyesi kudondoka chini.sehemu ambapo kinyesi kinadondokea pasiweze kufikiwa na kuku ,mara nyingi kinyesi hubeba vijidudu vya magonjwa.
Zingatia,
*nafasi inayopendekezwa kwa kuku 4 hadi 6 ianzie mita moja ya mraba .
Hili ni kwa ajili ya banda la kuku wakubwa miezi kuanzia miwili na nusu na kuendelea wapendwa kwa banda la kulelea vifaranga hadi muda mwingine.Mwenye ziada aongezee hapo kwenye comment .pia maoni weka hapo
……………………………………………………………………..