SEHEMU YA KWANZA
Tumerahisisha zaidi maelezo na kuifanya iakisi mazingira harisi ya mfugaji wa kitanzania
Ni mbinu ya kukuza mimea kwa kutumia mchanganyiko wa virutubisho vya madini katika maji bila kutumia udongo. Mchakato huu huchukua siku 6 hadi tisa kukamilika.
Kilo moja ya mbegu huzalisha wastani wa kilo 6 hadi kumi za majani na mizizi.
Faida za Teknolojia hii
i. Malisho huzalishwa ndani ya muda mfupi katika eneo dogo.mfano eneo la 4X3 mita huweza kutoa malisho sawa na ekari 2.
ii. Chakula hiki hulika chote kwa mifugo. Wanakula najani yote pamoja na mizizi. Hakuna upotevu wa chakula.
iii. Mahitaji ya maji ni madogo na maji yanaweza kutumika tena na tena.
iv. Gharama za uendeshaji wake ni mdogo; hakuna kuandaa ardhi, palizi na gharama za uvunaji.
v. Uwezekano mdogo sana wa wadudu ama magonjwa kushambulia.
i. Chakula hiki ni laini hivyo mmengényo wake katika mifugo ni mkubwa hivyo sehemu kubwa hutumika katika mwili wa mifugo na uzalishaji.
ii. Mazao ya mifugo uboreka zaidi na kuendana na mahtaji ya soko. Mfano:
 mayai ya kuku huwa na kiini cha njano zaidi wanapokula majani.
 Maziwa huwa na uwiano mzuri wa Omega 3 na Omega 6 amino acid ambazo hujenga afya imara ya mlaji.
iii. Hupunguza gharama za chakula na hivyo kuongeza faida.
iv. Virutubisho vingi hasa vitamin ambazo huchangia afya ya mifugo kuimalika.
v. Kinapolishwa kwa mchanganyiko na vyakula vingine kwa uwiano tutakaoutoa hapo mbele, uzalishaji na ukuaji wa mifugo huwa mzuri zaidi.
Vifaa mihimu
Sehemu/chumba cha kukuzia.
Nguzo na fito za kutengeneza chanja kwa ajili ya kupanga trei.
Trei za plastiki/aluminiamu.
Dawa yenye Chlorine (kama Waterguard) ama JIK kuua vijidudu katika maji na mbegu.
Virutubisho (nutrients): wengine hutumia buster za mazao (hakikisha haina madhara kwa mifugo).
Pump (sprayer) kunyunyiza maji.
Mbegu.
Mbegu zinazoweza kutumika
Shayiri, mahindi, ngano, mtama na nafaka nyingine nyingi.
SEHEMU YA PILI
UZALISHAJI WA MALISHO KWA TEKNOLOJIA YA HYDROPONIC
SEHEMU YA PILI
HATUA KWA HATUA KATIKA KUZALISHA HYDROPONIC
Kwa kufata hata hizi unaweza kuzalisha malisho yako mwenyewe nyumbani.
1. Chagua mbegu ambazo hazijaanza kuchipua, na hazina kemikali ama dawa ya aina yoyote.
2. Loweka mbegu katika mchanganyiko wa maji na Chlorine kwa masaa mawili kuepusha kuvu/uvundo ama vimelea vya magonjwa kumea na kukua.
3. Zitoe mbegu kwenye maji, zioshe kisha ziloweke kwenye maji safi kwa masaa 24 kuwezesha mbegu kufyonza maji vema.
4. Katika kupanda mbegu, pima kilo mbili za mbegu kwa kila trei yenye urefu wa Cm 80 kwa upana wa Cm 40.
5. Sambaza mbegu kwenye trei kwa usawa, (zisizidi Cm 3 kimo) ili kuwe na nafasi ya kutosha kwa kila mbegu kuchipua (kuota).
6. Hakikisha trei zina matundu kwenye kitako (chini) ambayo yamesambaa kwa usawa kuwezesha maji ya ziada kutoka.
7. Hamishia trei kwenye chanja ulizotengeneza. Mbegu zitaanza kuota katika hatua hii. Fanya hii ni siku ya kwanza.
8. Nyunyizia maji (kwa pampu) toka siku ya kwanza hadi ya sita, kwa mara nne katika kila masaa 24.
ZINGATIA.
Mbegu zenye dawa au sumu yoyote ni hatari kwa wanyama. zinaweza kuwadhoofisha ama kuwaua. hakikisha hautumii mbegu zenye dawa.
Jinsi ya kulisha
Kuku: kwa kuku 100 wanaotaga (layer) wape kilo 8 za hydroponics na waongezee kilo 4 za chakula cha ‘layer’ (layer mash) kwa siku.
Nguruwe: katika unenepeshaji wape kilo 2 za hydroponics na 1.5 za chakula kikavu (nafaka) kwa nguruwe mmoja kwa siku.
Ngómbe, mbuzi: wanaweza kutegemea majani haya tu na kuwa na uzalishaji mzuri bila nyongeza ya mchanganyiko wa nafaka. Kama uzalishaji wa maziwa ni mkubwa sana (zaidi ya lita 12 kwa siku) ni vema kuwaongezea nafaka.
Sungura: wanaweza kutegemea majani haya tu lakini ni vema kuwapa nyongeza ya mchanganyiko wa nafaka (angalau kwa uwiano wa 50%).
NUTRIENTS: wengine mliuliza kuhusu mbolea. mbolea ni adimu na bei kubwa. kwa uchunguzi tulioufanya BOOSTER ya mimea hasa yenye NPK inaweza kutumika kama mbadala wa nutrients. kama tulivyoeleza kwenye sehemu ya kwanza. booster ichanganywe na maji kabla ya kumwagilia.
matumizi ya nyungo unaweza kutumia ungo kupanda hyadroponi ila ni ghali kwa sababu ungo huoza haraka sababu ya unyevunyevu wakati wote hivyo ni muhimu kununua trei zinazodumu siku zote.
……………………………………………………………………………………………………………………………………………