Homa ya nguruwe (African swine fever) ni ugonjwa unaosababisha vifo vingi kwa nguruwe duniani kote. ugonjwa huu unasambaa kwa haraka sana.
Dalili za ugonjwa
Ugonjwa huu hushambulia na kuvuruga mfumo wa mzunguko wa damu, njia ya kupitisha chakula na njia ya kupumulia. unaweza kuziona dalili zake kuanzia siku tano hadi kumi na tano. Ugonjwa ukiwa mkali sana nguruwe wanaweza kufa hata kabla ya ugonjwa kuonekana.
Dalili za haraka ni nguruwe kukosa hamu ya kula na kupata homa kali kwa bahati nzuri mfugaji wa nguruwe anaweza kugundua vifo vya ghafla kwenye nguruwe wake. kwa wale nguruwe wanaobahatika kupona katika miili yao virusi vinakuwa vimebaki na vinaweza kutoka na kushambulia wenye afya nzuri.
Nguruwe aliyeathirika joto la mwili wake hupanda kutoka nyuzi za sentigedi 38.3 hadi 40 au zaidi ngozi yake huwa nyekundu kiasi kwa sababu ya homa matokeo ya shambulio kali ni nguruwe anaweza kufa baada ya siku sita mpaka ishirini cha ajabu nikwamba joto linalosababishwa na homa hupungua sana siku ya kwanza au tano kabla ya myama kufa.
Endapo maambukizi sio makali sana kunauwezekano walau nusu ya kundi la nguruwe wakanusuika kifo hata hivyo hao walionusurika hukaa na virusi mwilini mwao kwa miezi sita. Nguruwe walioambukizwa wanaweza kuonyesha dalili zifuatazo:-
.Kutokuwa mchangamfu
. kuvuja damu nyingi
. kupumua kwa shida
. kupenda kulala mara kwa mara
. pua imezungukwa na damu na foko la povu
. uharo mar kwa mara
. kuchujuka rangi sehemu mbalimbali za mwili
. kukohoa mara kwa mara
.tako limezungukwa na utando wa damudamu
.uharo wa damudamu
. Nyuma ya mapafu pamepakaa ute wa damudamu
. Mabaka mekundu sehemu za chini hadi ndani ya ngozi
. Ugiligili mwekundu umetanda ehemu za moyo
. Mabaka ya damu nyeusi sehemu za miguuni
. Utumbo mpana umejaa majitumbo na vidonda vyekundu
. Kibofu cha mkojo kimezingirwa na utando mweupe
. Kifuniko cha tumbo kkinarangi nyekundu
Dalili zinazo onekana baada ya kifo
Baada ya uchunguzi kufanyika na mtaalamu wa mifugo yafuatayo yanakuwa yamegundulika
. Mkusanyiko wa ugiligili kwenye fumbatio la tumbo
. Vidonda vinavyofanana na vya homa zinazosababisha magonjwa aina ya salmonellas, erysipelas na sumu nyinginezo
. kuvimba kwa damu na sehemu nyingine kutoka damu
. Vidonda vinavyosababisha na vya homa ya kawaida kwa nguruwe
Sehemu zinazohathiriwa sana na homa ya nguruwe ni;
. Ngozi hasa hasa kwenye masikio, pua, tumbo na mwisho wa sehemu za haja kubwa
. Bandama inaweza kuvimba hadi kufikia mara mbili ya tumbo lake la kawaida
. mapafu huwa na hali ya umajimaji pamoja na nimonia au kichomi
. Figo kutokwa damu sehemu chache chache au kiungo chote
. Mkusanyiko wa maji unaweza kuonekana kwenye vijishimo katika sehemu zingine mwilini au kwenye maungio wakati mwingine ugonjwa huu husababisha vifo vya ghafla hata kama dalili za vidonda hazikujitokeza.
.Uvimbevimbe kwenye limfu midhiri ya matone ya damu iliyoganda
Nkia zinazosababisha ugonjwa huu kuonea ni kama zifuatazo
Homa ya nguruwe ikitokea madhara ya kuenea kwa haraka sana. Chanzo chake ni nguuwe ambao tayari wameambukizwa shambulio likiwa kali sana, virusi vya ugonjwa huu huzagaa kwenye kinyesi, mkojo na jasho la nguuwe mwathirika.
Virusi hivyo vinaweza kuishi ndani ya uchafu huo kwa kipindi kirefu. Vilevile virusi hivyo vinaweza kuishi ndani ya nyama iliyohifadhiwa kwa muda wa siku 150 hivi.
Ifahamike kwamba nguruwe mwitu na ngiri waweza kubeba virusi hivi mwilini hata kama hawaonyeshindalili za kudhurika. Hatai ni kwamba virusi hivyo vikipata mwanya hufikisha mashambulizo kwa nguruwe wanaofugwa.
Uambukizaji waweza kufanyika kwa :-
.Mizoga iliyotupwa hovyo hovyo
.Kupitia kwa manyama poi waobeba virusi hivyo
.Kupitia kwenye kupe wanaobeba virusi hivi
. Mgusana kati ya nguruwe aliyeathirika na asiyehasirika
. Kupitia kwenye vitu visivyohai mathalani, viatu, nguo vifaa na magari
. Kupitia kwa wanyama pori wanaobeba virusi hivyo
Hatua zinazoweza kudhibiti ugonjwa huu
Hatua ya kwanza na muhimu ni kuhakikisha ugonjwa huu haungii kwenye mabanda ya nguruwe. Unaweza kufanikiwa hili kwa kutunza usafi mabandani na mazingira yanayozunguka.
Kila mara chunguza hali ya mifugo yako ukigundua dalili za magonjwa mwite mtaalamu wa mifugo haraka
Watenge ngurue wanaougua kasha hakikisha hawazururi ovyo nje ya banda.
Ukishuku kumezuka ghafula ugonjwa wa aina yoyote ile hakikisha mifugo ya aina yote haitangitangi ovyo shambani
Hakikisha watu na vyombo vya kusafiria havingii kiholela kwenye shamba la mifugo kama ni lazima zichukuliwe hatua za kiafya wakati wa kuingia na kutoka shambani au zizini.
Nguuwe wapya wakiletwa shambani, ni muhimu watengwe na wazamani kwa angalau siku 30
…………………………………………………………………………………………………………………..